Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Saturday, November 3, 2012

Waandamanaji Cairo wataka sheria za Kiislamu

Waandamanaji Cairo wataka sheria za Kiislamu Maelfu ya watu wamemiminika kwenye barabara za mji wa Cairo nchini Misri punde baada ya Sala ya Ijumaa wakitaka sheria za Kiislamu zitumiwe kuiongoza nchi.
Waandamanaji hao baadaye walikutana katika medani mashuhuri ya Tahrir huku wakipaza sauti na kusema 'Islamiya, Islamiya'. Harakati ya Ikhwanul Muslimin haikushiriki maandamano hayo ingawa baadhi ya duru zinasema kuwa huenda harakati hiyo pamoja na vyama vingine vya Kiislamu kama vile An-nur vikashirikiana na kuitisha maandamano makubwa ijumaa ijayo ili kushinikiza kutekelezwa sheria za Kiislamu.

Mjadala wa iwapo sheria za Kiislamu zijumuishwe kwenye katiba mpya ya Misri umekwamisha mchakato wa kuunda katiba hiyo kwani makundi yenye misimamo ya kiliberali yanataka nchi itawaliwe na sheria za kisekula badala ya sheria za Kiislamu.

No comments:

Post a Comment