Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo (UNDP)
limeeleza wasiwasi wake juu ya uwezekano wa kuzidi hali mbaya ya ukosefu
wa amani nchini Kenya kutokana na harakati za makundi ya wanamgambo
nchini humo.
Mkurugenzi mkaazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo nchini Kenya Maria-Threase Keating amesema kuwa UNDP ina wasiwasi kwamba kuenea kwa silaha nyepesi kati ya wananchi kutakwamisha juhudi za serikali ya Kenya za kufanyika uchaguzi wa amani.
Keating ambaye alikuwa akizungumza katika mkutano uliojadili maandalizi ya Kenya ya uchaguzi mkuu ujao amesema kuwa makundi yenye silaha katika maeneo ya vijijini iwapo yatashawishiwa huenda yakatumia silaha zao katika migogoro inayohusiana na uchaguzi.
Wataalamu wa masuala ya usalama wametangaza kuwa serikali ya Kenya inazembea katika kutekeleza mpango wa kukusanya silaha zinazomilikiwa na watu kote nchini hususan katika maeneo ya kaskazini na kaskazini magharibi mwa nchi hiyo.

No comments:
Post a Comment