Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Friday, November 30, 2012

Maalim Seif, Pinda waongoza mazishi mke wa Hamad Rashid

Viongozi mbali mbali wa vyama vya siasa na serikali wameshiriki katika mazishi ya bibi Kisa Mohd ambaye ni mke wa Mbunge wa Jimbo la Wawi (CUF) Mhe. Hamad Rashid Mohd.
Mazishi hayo yaliyofanyika nyumbani kwake Mikocheni jijini Dar es Salaam na kuzikwa katika makaburi ya kisutu, yaliongozwa na Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda na Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad.


Viongozi wengine waliohudhuria ni pamoja na Mwenyekiti wa CUF Prof. Ibrahim Lipumba, Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa UDP John Cheyo, Mwenyekiti wa ADC bw. Said Miraji na Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda.
Marehemu bibi Kisa Mohd alifariki Jumanne iliyopita ya tarehe 27/11/2012 baada ya kusumbuliwa na matatizo ya Presha kwa muda mrefu na kuzikwa jana tarehe 29/11/2012.
Akizungumza katika mazishi hayo, msemaji wa familia hiyo Profesa Matuja, amewashukuru viongozi na wananchi waliojitokeza kushirikiana nao katika msiba huo, na kwamba familia imepoteza mtu muhimu ambaye pengo lake linaweza kuchukua muda mrefu kuweza kuliziba.

No comments:

Post a Comment