Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Thursday, November 15, 2012

Hamas yasema Israel imejifungulia milango ya jahanam

Hamas yasema Israel imejifungulia milango ya jahanam
Brigedi ya Izzedin Qassam imetangaza kuwa utawala haramu wa Israel umejifungulia milango ya jahanam kwa kumuua shahidi kamanda wa brigedi hiyo Ahmed al Jabari katika hujuma huko Ukanda wa Ghaza. Jibril ambaye alikuwa kamanda wa Brigedi ya Izzedin Qassam Tawi la Kijeshi la Harakati ya Mapambano ya Kiislamu Palestina, Hamas ameuawa shahidi Jumatano ya leo katika hujuma zinazoendelezwa na utawala haramu wa Israel huko Ghaza.

Hamas imesema hujuma ya ndege za kivita  za Israel zimelenga Mji wa Ghaza, Rafah na Khan Yunis. Wapalestina wasiopungua tisa wameuawa katika hujuma hiyo ya utawala wa Kizayuni wa Israel huko Ghaza.
Wakati huo afisa moja wa Israel amesema mauaji ya kamanda huyo wa Izzedin Qssam ndio mwanzo wa hujuma mpya ya kijeshi dhidi ya Wapalestina huko Ghaza.

No comments:

Post a Comment