Umoja wa Mataifa umeitaka serikali
ya Myanmar kusitisha mara moja machafuko nchini humo. Msemaji wa Katibu
Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameeleza kutiwa wasiwasi na kuendelea machafuko
huko Myanmar na kuitaka serikali ya nchi hiyo kukomesha haraka
iwezekanavyo mashambulizi dhidi ya Waislamu wa nchi hiyo. Martin Nisirky
msemaji wa Ban Ki Moon Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ameashiria hali
ngumu inayowakabili wakimbizi wa Kiislamu wa Myanmar na kueleza kuwa
Umoja wa Mataifa unaitaka serikali ya nchi hiyo kusitisha mara moja
mashambulizi dhidi ya Waislamu na kuzingatia hali ya Waislamu wa nchi
hiyo. Nisirky amesema hali ni ya kutia wasiwasi huko katika mkoa wa
Rakhine na maelfu ya watu wameamua kuukimbia mkoa huo kupitia njia ya
majini na kwamba wamepata ripoti mbaya kuhusu hali za watu hao.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment