Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Friday, November 16, 2012

Nasrullah awataka watu huru kuwasaidia raia wa Gaza



Nasrullah awataka watu huru kuwasaidia raia wa GazaKatibu Mkuu wa harakati ya Hizbullah ya Lebanon Sayyid Hassan Nasrullah amewataka Waislamu, Waarabu na watu huru kote duniani kupigana bega kwa bega na watu wa Ukanda wa Gaza dhidi ya utawala ghasibu wa Israel.
Sayyid Nasrullah ambaye alikuwa akizungumzia mashambulizi ya sasa ya Israel dhidi ya watu wa Gaza amesema yanayotokea sasa katika eneo hilo ni mpambano baina ya utawala unaopenda kumwaga damu za watu wa Israel na mataifa ya Mashariki ya Kati hususan Wapalestina. Amesema watawala katili wa Tel Aviv hawahitaji sababu yoyote kwa ajili ya kutekeleza ukatili na kusisitiza kuwa viongozi hao wameshtushwa na uwezo wa kujihami wa makundi ya wapigania uhuru wa Palestina. Amesema majibu ya makombora ya makundi ya jihadi ya Palestina dhidi ya mji wa Tel Aviv yamewaacha bumbuazi Wazayuni na kudhihirisha uwezo wa wanamapambano wa Kipalestina.
Katibu Mkuu wa Hizbullah amewataka viongozi wa kisiasa wa Mashariki ya Kati kutupilia mbali hitilafu zao na kuungana kwa ajili ya kujibu uchokozi wa adui Mzayuni huko katika Ukanda wa Gaza.
Wapalestina wasiopungua 19 wameuawa shahidi katika mashambulizi yanayoendelea kufanywa na jeshi la Israel dhidi ya raia wa Gaza.

No comments:

Post a Comment