Harakati ya Jihadul Islami ya
Palestina imesema kuwa, kuna udharura wa Misri kusimamia utekelezwaji wa
makubaliano ya maridhiano ya kitaifa kati ya makundi ya Palestina.
Khalid al Batwash afisa mwandamizi wa harakati ya Jihadul Islami ya
Palestina amesema hayo leo alipokutana na maulamaa wa Misri katika
Ukanda wa Gaza na kuwataka viongozi wa Cairo kupatanisha katika suala la
utekelezaji makubaliano ya maridhiano ya kitaifa kati ya harakati ya
Fat'h na Hamas.
Amesisitiza kuwa, kuendelea hitilafu
kati ya makundi ya Palestina ni kwa manufaa ya adui Mzayuni. Viongozi wa
harakati hizo mbili za Palestina Februari 5 mwaka huu walitia saini
mjini Doha, Qatar makubaliano ya kuweka kando hitilafu zao kwa lengo la
kuunda serikali ya umoja wa kitaifa na kuitisha uchaguzi, lakini hadi
sasa makubaliano hayo bado hayajatekelezwa.
No comments:
Post a Comment