Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Friday, November 16, 2012

AU: Serikali ya Mali ifanye mazungumzo na waasi



AU: Serikali ya Mali ifanye mazungumzo na waasiUmoja wa Afrika umeitaka serikali ya Mali kufanya mazungumzo na makundi ya waasi nchini humo.
Mwakili wa ngazi za juu wa Umoja wa Afrika katika mauala ya Mali Pierre Buyoya ameitaka serikali ya Mali kufanya juhudi kubwa zaidi za kufanya mazungumzo na makundi ya waasi wanaobeba silaha huko kaskazini mwa nchi hiyo.
Buyoya amesema iwapo serikali ya Bamako itaanza mazungumzo na makundi yenye silaha waasi wa makundi mengine watapoteza uwezo wa kukabiliana na jeshi la serikali.
Wito huo wa Pierre Buyoya umetolewa baada ya mazungumzo ya Rais wa Burkina Faso Blaise Compaore ambaye ni mpatanishi katika mgogoro wa kaskazini mwa Mali na mwakilishi wa kundi la Ansaruddin ambaye ameyataka makundi mengine ya waasi kufanya mazungumzo na serikali ya Bamako.
Mwakilishi wa kundi la waasi la Ansaruddin amesema makundi yote ya Mali yanaweza kujadili njia za kukomesha hitilafu zilizopo kupitia mazungumzo ya kisiasa baada ya kukomeshwa machafuko ya sasa.
Makundi ya waasi ya Mali yalilidhibiti eneo la kaskazini mwa nchi hiyo baada ya mapinduzi ya kijeshi yaliyofanyika nchini humo tarehe 22 Machi mwaka huu.

No comments:

Post a Comment