Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa ametoa wito wa kukomeshwa vitendo
vya utumiaji mabavu na kuwanyanyasa wanawake. Ban Ki Moon amesema hayo
katika risala yake kwa mnasaba wa Novemba 25, Siku ya Kimataifa ya
Kupambana na Unyanyasaji wa Wanawake. Ban Ki Moon amesema, licha ya
kuweko hatua zilizochukuliwa za kupambana na unyanyasaji dhidi ya
wanawake, asilimia 70 ya wanawake hukabiliwa na vitendo vya utumiaji
mabavu na unyanyasaji wa kijinsia katika kipindi cha maisha yao na
kwamba, robo ya wanawake huwa ni wajawazito. Katibu Mkuu wa Umoja wa
Mataifa amesema, utumiaji mabavu dhidi ya wanawake ni misdaqi ya wazi ya
ukiukaji wa haki za binadamu na kwamba, nchi zanachama za umoja huo
zinapaswa kuandaa mipango na mikakati ya kung'oa mizizi ya vitendo hivyo
vibaya.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment