Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Friday, November 23, 2012

Wanne wauawa kwenye maandamano nchini Nigeria



Wanne wauawa kwenye maandamano nchini Nigeria
Watu wasiopungua wanne wameuawa na makumi ya wengine kujeruhiwa, baada ya kutokea ghasia kati ya jeshi la polisi na waandamanji huko kaskazini magharibi mwa Nigeria. Taarifa zinasema kuwa, kundi la Waislamu katika mji wa Bichi katika jimbo la Kano kaskazini magharibi mwa Nigeria lilimiminika barabarani
hapo jana kupinga hatua ya kuvunjiwa heshima matukufu ya Kiislamu nchini humo. Ibrahim Idris  Kamanda wa Polisi  katika jimbo la Kano amedai kuwa, mapigano hayo kati ya polisi na waandamanaji yametokea baada ya  Waislamu wa eneo hilo kusikia taarifa kwamba kuna vitendo vimefanyika vyenye kuyavunjia heshima matukufu ya Kiislamu. Kamanda Ibrahim Idris ameeleza kuwa, inasemekana Muislamu mmoja wa mji wa Bichi alisikia kauli ya mfuasi mmoja wa Kikristo wa nchi hiyo akimvunjia heshima na kumdhihaki Mtume Mtukufu SAW, kitendo ambacho kiliwakasirisha Waislamu na hatimaye kuchukua uamuzi wa kumiminika barabarani.

No comments:

Post a Comment