Baraza la Seneti la Marekani liko katika mikakati ya
kuweka vikwazo vipya vya kiuchumi dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran,
ikiwemo kuzuia fedha zote zinazofungamana na Taasisi ya Redio na
Televisheni ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran IRIB. Taarifa zinasema kuwa,
vikwazo hivyo vipya vya Marekani dhidi ya IRIB ni mwendelezo wa njama za
nchi za Magharibi na hasa Marekani za kuvinyamazisha vyombo vya habari
vya hapa nchini. Taarifa hiyo imeeleza kuwa,
mkakati huo wa Seneti ya
Marekani pamoja na hatua za hivi karibuni za wakuu wa Eutelsat na
Intelsat za kukataa kurusha kupitia satalaiti zao vipindi vya kanali
mbalimbali za televisheni na redio za Iran mwezi uliopita, ni ukiukaji
wa wazi wa uhuru wa kujieleza na kupasha habari. Kusitishwa urushwaji wa
matangazo hayo kwenye satalaiti hizo kulitokana na mashinikizo ya wakuu
wa nchi za Umoja wa Ulaya. Mwanzoni mwa mwezi huu, satalaiti ya Asiasat
iliyoko Hong Kong nayo pia ilisimamisha kurusha hewani matangazo ya
redio na televisheni za Iran kutokana na mashinikizo ya Marekani. Hali
kadhalika, Marekani imeshaiwekea vikwazo Iran katika sekta za mafuta,
nishati, bandari na mashirika ya meli. Mwendelezo wa vikwazo vya nchi za
Magharibi na hasa Marekani dhidi ya Iran unatokana na madai yao potofu
kwamba Iran ina mpango wa kutengeneza mabomu ya nyuklia, amma viongozi
wa Tehran na hata Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Nyuklia IAEA
wamesisitiza mara kadhaa kwamba mpango wa nyuklia wa Iran unafanyika kwa
malengo ya amani tena chini ya usimamizi wa wakaguzi wa IAEA.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment