Dk. Juma Salum Mambi ambae ni Katibu wa Jumuiya ya Madaktari, akifafanua jambo kwa wajumbe kuhusu katiba yao
.………………………………………………………
Na Fatma Mzee, Maelzeo
JUMUIYA ya Madaktari
Zanzibar, imefanya mkutano wa kujadili katiba yake kwa lengo la
kuifanyia marekebisho ili iende na wakati wa sasa.
Miongoni mwa marekebisho hayo, ni pamoja na kuongeza kipengele cha jumuiya hiyo kuwa na mwanasheria wake.
Mwenyekiti wa jumuiya
hiyo ambaye ndiye aliyeongoza mkutano huo Dk. Said Mohamed Abdullah,
aliwashauri wanachama kuisoma vyema katiba hiyo na kuainisha maeneo
wanayohisi yanahitaji kurekebishwa ili kuiimarisha zaidi .
Alisisitiza
umuhimu kwa wanachama kutopuuza kuhudhuria na kufuatilia vikao kwa
lengo la kuwa na jumuiya iliyo imara na inaweza kusimamia vizuri
matarajio yao.
Hata
hivyo, wajumbe wote wa jumuiya hiyo walikubaliana na katiba hiyo,
ingawa baadhi yao waliomba wapatiwe muda zaidi wa kuipitia kwa kina
kabla kutoa mapendekezo yao.
Mjumbe
mmoja Yussuf Haji, aliwaomba wanachama wenzake kuiheshimu katiba hiyo,
kwani ndio muongozo utakaowezesha kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.
Kwa
upande wake, Katibu wa jumuiya hiyo Dk. Juma Salum Mambi alisema, ili
jumuiya hiyo ifanikiwe na na kufanana na jumuiya nyengine zilizopiga
hatua kubwa, ni vyema madaktari wazingatie haja ya kuzidi kuonesha umoja
na mshikamano utakaosaidia kuiimarisha jumuiya yao.
Mkutano huo umeakhirishwa hadi Disemba 8, mwaka huu ili kutoa fursa kwa wanachama kuipitia kikamilifu katiba hiyo.
No comments:
Post a Comment