Askari polisi wasiopungua 29 wameuawa nchini Kenya baada ya
kutokea mapigano kati ya watu wanaobeba silaha na askari polisi katika
eneo la kaskazini mwa nchi hiyo. Tarifa zinasema kuwa, mapigano hayo
yamejiri kati ya askari polisi na kundi la watu wanaobeba silaha katika
wilaya ya Baragoi iliyoko kaskazini mwa Kenya na kupeleka askari polisi
hao kuuawa na wengine zaidi ya 21 kujeruhiwa, wakiwa kwenye operesheni
ya kutafuta ng'ombe. Jeshi la Polisi nchini Kenya limethibitisha kuuawa
askari polisi hao 29 katika shambulio hilo la watu wanaobeba silaha.
Hayo yanahesabiwa kuwa ni mauaji makubwa zaidi kufanywa dhidi ya askari
polisi tokea nchi hiyo ilipojinyakulia uhuru wake karibu miaka 50
iliyopita.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment