Kasambara amekwenda mbali ambapo pia ameiamuru polisi kutowakamata mashoga. Kiongozi huyo amesema wananchi watatoa maoni yao kuhusu hatima ya sheria hiyo.
Uchunguzi wa maoni uliofanywa na gazeti moja la kila siku nchini Malawi unaonyesha kuwa, zaidi ya asilimia 80 ya wananchi wanapinga hatua hiyo ya serikali na wanataka sheria hiyo iendelee kufanya kazi.
Kwa mujibu wa sheria hiyo, ngono kati ya watu wa jinsia moja ni hatia na adhabu yake si chini ya miaka 14 jela pamoja na faini kubwa.
Mwaka 2009, mashoga 2 walihukumiwa kifungo cha miaka 14 jela nchini Malawi lakini hukumu hiyo ikabatilishwa baada ya mashinikizo ya kila upande kutoka nchi za Magharibi. Hatua ya hivi sasa ya kusimamishwa utekelezaji wa sheria dhidi ya ushoga inatilia shaka misimamo ya Rais Joyce Banda wa nchi hiyo kuhusu masuala muhimu hususana yanayohusu maadili ya Kiafrika.
No comments:
Post a Comment