Bunge la Somalia limepasisha baraza jipya na dogo la mawaziri wa serikali mpya ya nchi hiyo.
Baraza la mawaziri 10 la serikali ya Waziri Mkuu wa Somalia Abdi Farah Shirdon lina wanawake wawili ambao mmoja wao amepewa mkoba wa Wizara ya Mambo ya Nje.
Msemaji wa Bunge la Somalia Mohmed Sheik Osman Jawari amesema bunge hilo limepasisha kwa kura nyingi baraza jipya la serikali na kwamba wabunge 219 kati ya 225 waliokuwepo bungeni wamewapigia kura ya ndio mawaziri hao.
Mjumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Somalia Augustine Mahiga amepongeza zoezi hilo hususan kupasishwa wanawake wawili kuwa mawaziri katika serikali mpya ya Somalia na kusema ni hatua muhimu katika historia ya Somalia.
Mawaziri wa serikali mpya ya Somalia wanatazamiwa kuapishwa wiki ijayo.

No comments:
Post a Comment