Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Tuesday, November 27, 2012

Israel yatuhumiwa kuwa ilifanya jinai za kivita Gaza


Israel yatuhumiwa kuwa ilifanya jinai za kivita GazaJumuiya ya Kimataifa ya Amani ya Kiislamu leo imetoa taarifa mjini Tehran ikitangaza kuwa mashambulizi ya kijeshi ya utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Ukanda wa Gaza ni tishio kwa amani na usalama wa Mashariki ya Kati.
Jumuiya hiyo pia imeitaka jamii ya kimataifa ikiwemo Kamati ya Kimataifa ya Msalaba Mwekundu kukomesha jinai za Israel kwa kuchukua hatua za dharura za kuwalinda watu wa Gaza na kuunda muungano wa kimataifa wa kulilinda eneo hilo.
Taarifa ya Jumuiya ya Kimataifa ya Amani ya Kiislamu imesisitiza kuwa mashambulizi ya jeshi la Israel dhidi ya raia na kuharibu makazi ya watu wa Gaza ni jinai ya kivita.
Wapalestina wasiopungua 175 wameuawa shadhidi na wengine 1400 kujeruhiwa katika mashambulizi yaliyofanywa na jeshi la Israel dhidi ya Ukanda wa Gaza kuanzia tarehe 14 hadi 21 Novemba mwaka huu.

No comments:

Post a Comment