Waasi wa mashariki mwa Kongo DRC wamesema kuwa wanaanza kuondoka
katika mji waliouteka wa Goma, ikiwa ni siku kadhaa baada kufikia
makubaliano na serikali kwa upatanishi wa Uganda. Amani Kabashi msemaji
wa waasi wa M23 amesema kuwa, wanaanza kundoka katika mji wa Masisi
ulioko kilomita 50 kutoka katika jiji la Goma, kisha wataondoka katika
eneo la Sake na mwishowe wataondoka kikamilifu katika mji wa Goma. Hii
ni katika hali ambayo Herve Ladsous, Mkuu wa askari wa kulinda amani wa
Umoja wa Mataifa huko Kongo amethibitisha kuwa waasi hao wameacha
kusonga mbele na kwamba kuna dalili za kuondoka katika mji wa Goma.
Wakati huo huo Jean Marie Runinga, kiongozi wa kisiasa wa waasi wa M23
amesema, kundi hilo halipingi kuondoka katika mji wa Goma, na kwamba
bila ya shaka yoyote litafanya hivyo baada ya kutekelezwa masharti yake.
Amesema, miongoni mwa masharti ya waasi hao ni kuachiliwa huru Etienne
Tshisekedi, kiongozi wa upinzani aliyewahi kuwa Waziri Mkuu wa Kongo.
Tshisekedi anashikiliwa katika kifungo cha nyumbani tangu
alipojitangazia ushindi baada ya uchaguzi wa rais wa mwaka uliopita
ambapo Rais Joseph Kabila alitangazwa mshindi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment