Serikali za Tanzania na Malawi zimefikia makubaliano ya kumtafuta
 mpatanishi wa kimataifa atakayetatua hitilafu za mpaka wa majini kati 
ya nchi hizo mbili. Bernard Membe Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa 
Tanzania ameyasema hayo mjini Dar es Salaam alipokutana na mwenzake 
Ephrahim Muganda Chiume wa Malawi na kuongeza kuwa, pande hizo mbili 
zimechukua uamuzi wa pamoja wa kuupeleka mgogoro huo kwa jopo la maraisi
 wastaafu wa Afrika linaloongozwa na Joaquim Chissano Rais wa zamani wa 
Msumbiji ambalo linashughulikia kutatua hitilafu na migogoro mbalimbali 
barani  Afrika.
Pande hizo mbili zimeafikiana kwamba, iwapo hazitaridhishwa na maamuzi ya upatanishi huo, zitalazimika kuwasilisha hitilafu zao kwenye Mahakama ya Kimataifa ya Haki ICJ. Malawi inadai kwamba mpaka wa nchi hizo mbili upo kwenye ufukwe wa Tanzania kwa maana kwamba nchi hiyo haina haki ya kutumia maji ya ziwa hilo ambalo linahesabiwa kuwa ni la tatu kwa ukubwa barani Afrika. Hii ni katika hali ambayo, Tanzania nayo inadai kuwa mpaka wa nchi hizo mbili uko katikati ya maji ya ziwa Nyasa. Mgogoro kati ya Tanzania na Malawi ulianza mwezi Julai mwaka huu baada ya Malawi kuanza kufanya utafiti wa mafuta katika eneo la Tanzania, hali ambayo ilisababisha serikali hizo mbili kuanza kulumbana. Inasemekana kuwa, chini ya maji ya ziwa hilo kuna utajiri mkubwa wa mafuta na gesi.
   
No comments:
Post a Comment