skip to main |
skip to sidebar
Mauritania yaonya athari za uingiliaji kijeshi Mali
Spika wa bunge la Mauritania amesema kuwa uingiliaji kijeshi huko
Mali kwa ajili ya kukabiliana na makundi yanayobeba silaha huko
kaskazini mwa nchi utakuwa na mripuko mkubwa wa volcano kwa eneo zima
la sawa Sahel la Afrika. Masoud Ould Bilkhair Spika wa bunge la
Mauritania amesema kuwa vita dhidi ya makundi yenye silaha huko
kaskazini mwa Mali vitakuwa na atahari mbaya kwa nchi jirani na Mali.
Spika wa bunge la Mauritania amesisitiza kuwa viongozi wa Bamako
wanapasa kwanza kufanya juhudi ili kuutatua kwa amani mgogoro wa
kaskazini mwa nchi hiyo ilikuweza kulinda umoja wa ardhi nzima ya Mali
na kudumisha demokrasia nchini humo.
No comments:
Post a Comment