Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Tuesday, November 13, 2012

Ash Shabab waua watu 11 Mogadishu, Somalia

Ash Shabab waua watu 11 Mogadishu, Somalia
Watu wasiopungua 11 wameuawa na wengine 15 kujeruhiwa baada ya wanamgambo wa ash Shabab kufanya mashambulizi ya kushtukiza kwenye kambi moja ya kijeshi ya mji mkuu wa Somalia, Mogadishu.
Mashambulizi hayo yametokea katika eneo la Elasha Biyaha nje ya mji wa Mogadishu na kupelekea watu wasiopungua 10 kuuawa wakiwemo wanajeshi watatu na raia saba.

Afisa wa kijeshi wa Somalia, Kanali Abdullahi Caabi, amethibitisha habari ya kutokea mashambulizi hayo na hasara zake.
Mashambulio hayo ya ash Shabab yamekuja huku wanajeshi wa Umoja wa Afrika pamoja na wale wa serikali ya Somalia wakiwa wamesema kuwa, tarehe 25 mwezi uliopita wa Okroba waliwatia mbaroni wanamgambo wasiopungua 62 wa ash Shabab wakiwemo makamanda wa kundi hilo katika operesheni walioifanya kwenye maeneo hayo hayo.

No comments:

Post a Comment