Uwekaji wa Nguzo za kupitishia waya mpya wa Umeme unaotokea Ras
Kilomoni hadi Ras Fumba zikiwa tayari zimeshaweka katika eneo
litakalopita waya huo kama inavyoonekana nguzo hizo zikiwa katika maeneo
yato yanayotakiwa kupita waya huo.
Nguzo hizi zikiwa katika maeneo ya Maungani zikielekea Mtoni tayari kwa
kiasi kikubwa uwekaji wa nguzo hizo umekamilika ukisubiri kuwekwa waya.
Maendeleo ya teknolojia yanaonekana kwa kuwepo tofauti kati ya nguzo za
zamani na hizi mpya ambazo zimepitishwa katika njia ile ile iliyopita
waya ya zamani.
Umeme huu unatarajiwa kuanza kutumika Mwezi Desemba 2012 baada ya waya wa zamani kumaliza muda wake wa miaka 30.
No comments:
Post a Comment