Viongozi wa Uswisi wameeleza
wasiwasi wao wa kuongezeka wimbi la magendo ya madawa ya kulevya nchini
humo. Polisi wa kupambana na magendo ya madawa ya kulenya nchini Uswisi
wameeleza kuwa, mji wa Zurich kwa kushirikiana na Idara ya kupambana na
madawa ya kulevya ya Nigeria wameweka mikakati ya kuwasaka na kuwatia
mbaroni raia wa Nigeria wanaofanya biashara hiyo haramu nchini humo.
Mkuu wa Idara ya Kupambana na Madawa ya Kulevya nchini Uswisi amesema
kuwa, biashara ya kokeini inashikiliwa na wafanyabiashara wa Nigeria
nchini humo. Naye Afisa wa Nigeria amesema kuwa, maafisa wa Uswisi
hawana mikakati madhubuti ya kupambana na wafanya magendo wa madawa ya
kulevya.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment