Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Friday, November 23, 2012

Tanzania kuanzisha kadi za simu za mkononi zinazoweza kutumika kwa mitandao tofauti


Serikali ya Tanzania itaanzisha mfumo wa kadi za namba za simu za mkononi zinazoweza kutumika kwa mitandao tofauti mwaka ujao ambao utawawezesha watumiaji kuhifadhi namba zao za simu wakati wanapobadilisha kutoka kwa mtoa huduma mmoja kwenda kwa mwingine, kwa mujibu wa Mamlaka ya Sheria za Mawasilaino Tanzania (TCRA).
  • Mteja akijadilana na muuzaji wa simu za mkononi katika duka la Tecno katika maeneo ya Kariakoo jijini Dar es Salaam tarehe 17 mwezi Novemba. [Deodatus Balile/Sabahi] Mteja akijadilana na muuzaji wa simu za mkononi katika duka la Tecno katika maeneo ya Kariakoo jijini Dar es Salaam
"Wateja hawataendelea kushikiliwa kwa mtoa huduma mmoja," Mkurugenzi Mtendaji wa TCRA John Nkoma aliiambia Sabahi. "Kwa kutumia mfumo huu unaweza kubadilisha watoa huduma wakati unapotaka kutegemeana na ubora na gharama."

Alisema mfumo mpya utawawezesha wateja kuingia kwenye namba zao kutoka mtandao mmoja kwenda mwingine kwa kutumia kadi ya SIM ile ile pamoja na namba zake za mawasiliano zikiwa vilevile. Kwa sasa, ubadilishaji wa mtandao mmoja kwenda mwingine unahitaji kununua kadi ya SIM mpya zenye namba tofauti na wakati mwingine simu ya pili.
"Kupoteza namba ni kikwazo kikubwa kwenye kubadilisha mitandao kwa namba za wateja," Nkoma alisema.
Uwezekano wa kutumia kadi moja kwa mitandao tofauti ya simu za mkononi awali ulipangwa kuanza mwezi huu, lakini makampuni ya simu yaliomba miezi mitatu ili kurekebisha miundombinu yao.
Nkoma alisema uwezekano wa kutumia namba nyingi utaongeza ushindani miongoni mwa watoa huduma, hatimaye kuongeza ubora wa huduma na kupunguza gharama kwa sababu watoa huduma watalazimika kubadilisha upangaji gharama kama watataka kubakia na wateja wao.
Mabadiliko mengine yatakuwa ada ya kutumia mtandao mwingine tofauti itakayotozwa wakati wa kupiga simu baina ya makampuni tofauti ya simu za mkononi. TCRA imeweka kikomo cha juu cha ada ya kutumia mtandao mwingine tofauti, lakini makampuni yanayotoa huduma yanaweza kutoza chini ya hapo.
Kwa sasa, baadhi ya wateja wanatumia hadi simu nne za mkononi kutoka kwa makampuni tofauti ya simu ili kuepuka ada ya kutumia mtandao mwingine, Nkoma alisema, kwa kila simu kutumika kupiga simu zenye namba za mtandao unaofanana.
Ratifa Ali, anayeuza vifaa vya elektroniki Dar es Salaam, alisema ana wasiwasi mfumo mpya utapunguza mauzo katika duka lake.
"Kimsingi wauzaji wote wa simu za mkononi watapoteza biashara," aliiambia Sabahi. Kama upinzani kati ya watoa huduma itawasababisha kushusha ada ya uunganishaji wa mitandao, watumiaji hawatanunua tena simu nyingi, alisema.
Lakini Babu Masola, mmiliki wa duka la simu za mkononi huko Dar es Salaam, alisema kushuka kwa mauzo ya simu za bei rahisi kunawezekana kufidiwa na mauzo ya simu zinazodumu. Kwa kuwa na uwezekano wa kutumia kadi moja kwa mitandao tofauti, wateja watanunua zaidi simu za bei ya juu kwa sababu watakuwa na uwezo wa kutumia simu moja kwa mitandao yote, alisema.
Aristides Majura, mkazi wa Dar es Salaam, alisema kuanzishwa kwa uwezekano wa kutumia kadi moja kwa mitandao tofauti kutawapa uhuru wafanyabiashara kufuata biashara yenye faida bila kuathiri biashara zao.
Alisema huduma kwa baadhi ya watoa huduma ni za gharama ya juu sana, lakini watumiaji wa biashara hizo wanaogopa kubadilisha watoa huduma na kubadilisha namba zao kwa sababu wanaweza kuwapoteza wateja.
"Unapobadilisha watoa huduma, unapoteza mawasiliano na wakati mwingine biashara, kwani hakuna uwezekano wa kuwapigia wateja wote kuwafahamisha kwamba umebadilisha namba ya simu," alisema. "Lakini sasa kwa kutumia teknolojia hii unafuata kwenye huduma nzuri kwa kutumia namba yako ya asili. Hii ni nzuri sana!"

No comments:

Post a Comment