Waasi wa jimbo lenye utajiri mwingi wa mafuta nchini Sudan,
wametangaza leo kuwa wameiangusha ndege ya kijeshi aina ya Antonov ya
nchi hiyo katika jimbo la Kordofan kusini nchini Sudan. Duru za habari
zimenukuu ripoti ya waasi wa Harakati ya Ukombozi ya Wananchi wa Sudan
(SPLA) tawi la kaskazini ikidai kuwa, harakati hiyo iliiangusha ndege
hiyo ya kijeshi katika majira ya saa 11 jioni kwa majira ya eneo hilo,
katika
eneo la Jau huko Kordofan Kusini karibu na mpaka na Sudan Kusini. Hata hivyo habari hiyo haijathibitishwa na duru rasmi za jeshi la Sudan. Jeshi la Ukombozi la Wananchi wa Sudan (SPLA) limekuwa likitekeleza mashambulizi ya mara kwa mara katika siku za hivi karibuni, kama radiamali yake dhidi ya mashambulizi ya anga yanayofanywa na jeshi la Sudan kuvilenga vijiji vya eneo la Kordofan.

No comments:
Post a Comment