Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Sunday, April 21, 2013

Wabahrain wapinga mashindano ya langa-langa


Waandamanaji Bahrain wakiwa na vibonzo vinavyoonyesha namna mashindano ya langa-langa yatakavyosaidia ukandamizajiVikosi vya kijeshi Bahrain vimetumia gesi ya kutoa machozi kuwatawanya waandamanaji wanaopinga kufanyika mashindano ya magari ya langa-langa ya Formula One Grand Prix ambayo yanatazamiwa kuanza leo katika mji mkuu, Manama.
Watu wa Bahrain wanataka mashindano hayo yasimamishwe kwa sababu utawala wa ukoo wa Aal Khalifa unakandamiza maandamano ya amani ya wanaotaka mabadiliko nchini humo. Wabahrain wanasema utawala wa kifalme unataka kutumia mashindano hayo ya langa-langa kuonyesha kila kitu ni shwari katika nchi hiyo ndogo ya Ghuba ya Uajemi.
Kwa miaka miwili sasa Bahrain imekumbwa na mgogoro mkubwa uliosababisha mashindano hayo ya magari yasifanyike mwaka 2011. Mwaka 2012 utawala wa Aal Khalifa ulifanya mashindano hayo kwa kustafidi na uungaji mkono wa vikosi vya usalama vya Saudia. Lakini mwaka huu wananchi na wapinzani wa Bahrain wamesisitiza kuendelea na malalamiko yao dhidi ya hatua kama hizo za kimaonyesho, licha ya ukandamizaji wa utawala wa kifalme wa Aali Khalifa.

Nigeria yaanzisha kampeni dhidi ya uvumi


Bango linalowaonyesha watu wakipashana uvumi na maandishi yanayo toa wito kwa Wanigeria 'kusema la kwa waeneza uvumi'
Wakuu wa jimbo lenye utajiri wa mafuta la Bayelsa nchini Nigeria wameanzisha kampeni maalamu yenye kauli mbiu ya 'sema la kwa waeneza uvumi'.
Kampeni hiyo imeanzishwa kufuatia kuibuka taharuki baada ya kuenea uvumi kuwa gavana wa jimbo hilo amefutwa kazi. Katika mabango yaliyowekwa barabarani Wanigeria wanahimizwa kutosikiliza uvumi wala kuuhimiza. Wanaoendesha kampeni hiyo wanasema uvumi umeathiri vibaya utendaji kazi katika jimbo hilo.
Msemaji wa gavana wa jimbo hilo Daniel Iworiso-Markson amewaambia waandishi habari kuwa kampeni hiyo haina lengo la kuwanyima watu uhuru wa maoni. Ili kukabiliana na tatizo la uvumi katika jamii, wakuu wa jimbo hilo wamebuni kamati ya wataalamu watakaowaelimisha watu kuhusu uovu wa kueneza uvumi. Aidha serikali ya jimbo hilo imetangaza nambari maalumu za simu ili kila mwenye kutaka habari rasmi azipate kupitia njia hiyo badala ya kutegemea uvumi. Jimbo la Bayelsa ni nyumbani kwa Rais Goodluck Jonathan wa Nigeria.

Mufti wa Tunisia: Vita dhidi ya serikali ya Syria si Jihad


Mufti wa Tunisia Sheikh Othman BattikhMufti wa Tunisia Sheikh Othman Battikh amesema wito wa Jihad dhidi ya serikali ya Syria si sahihi kwa mujibu wa sheria za Kiislamu na ni kosa kubwa.
Akizungumza na waandishi habari siku ya Ijumaa, mwanazuoni huyo wa ngazi za juu Tunisia amesisitiza kuwa, 'Mwislamu hapaswi kupigana dhidi ya Mwislamu mwenzake' kwa kisingizio chochote kile.
Sheikh Battikh ametoa matamshi hayo baada ya kubainika kuwa vijana wengi wa Tunisia wanajiunga na mitandao ya kigaidi inayowatuma Syria kupigana dhidi ya serikali halali ya Rais Bashar al-Assad. Mwanazuoni huyo wa Tunisia aidha amesema kile ambacho sasa kinajulikana kama 'jihad ya ngono' ni zinaa na ukahaba. Amesema wasichana wadogo wa Tunisia wenye umri wa miaka 16 wamehadaiwa na kuenda Syria kushiriki katika kile Mawahabi wanakitaja kuwa ni ngono au ndoa ya jihad.

Monday, April 15, 2013

OIC yataka kutuma kamati yake nchini Myanmar


OIC yataka kutuma kamati yake nchini MyanmarJumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu OIC imetoa wito wa kutumwa kamati ya jumuiya hiyo nchini Myanmar kwa shabaha ya kushuhudia kwa karibu hali inayowakabili Waislamu wa jamii ya Rohingya wa nchi hiyo. Taarifa ya mwisho ya mkutano wa kamati ya mawasiliano ya OIC imeitaka serikali ya Myanmar kuruhusu kamati ya mawaziri ya jumuiya hiyo kutumwa katika nchi hiyo. Akizungumza katika mkutano huo, Profesa Ekmeleddin İhsanoğluKatibu Mkuu wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu OIC amesema kuwa, utumiaji mabavu unaofanywa dhidi ya Waislamu wa Myanmar haukubaliki hata kidogo na kwamba, hiyo ni ishara ya utendaji mbaya wa serikali ya nchi hiyo. Ni mwaka mmoja sasa ambapo OIC imekuwa ikitaka kutuma kamati ya uchunguzi nchini Myanmar lakini bado haijafanikiwa hadi sasa. Katika taarifa yake, Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu OIC imeitaka Kamisheni ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa kutuma timu ya uchunguzi nchini Myanmar. Aidha OIC imezitaka nchi jirani na Myanmar kama Bangladesh na Malaysia kusaidia kutatua tatizo la Waislamu wa Rohingya wanaoandamwa na wimbi la mauaji yanayofanywa na Mabudha wenye misimamo mikali wakishirikiana na askari wa jeshi la serikali ya Myanmar.

Na Salum Bendera

Watu 20 wauawa katika machafuko C.A.R.


Watu 20 wauawa katika machafuko C.A.R.Watu wasiopungua 20 wameuawa katika Jamhuri ya Afrika ya Kati na makumi ya wengine kujeruhiwa baada ya kuzuka machafuko katika mji mkuu wa nchi hiyo Bangui. Duru za hospitali, polisi na mashuhuda wanasema kuwa, watu hao wameuawa katika mapigano na machafuko tofauti yaliyotokea katika mji wa Bangui. Taarifa zaidi zinasema kuwa, watu 12 wameuawa katika Wilaya 7 za mji mkuu Bangui huku Shirika la Msalaba Mwekundu likiongeza kuwa, watu wengine wanne wameuawa katika maeneo mengine ya mji huo. Polisi imesema kuwa, mapigano hayo yalizuka wakati wanachama wa muungano wa waasi wa Seleka walipokuwa wakisaka silaha baina ya raia. Hayo yanajiri katika hali ambayo, Baraza la Mpito katika Jamhuri ya Afrika ya Kati limemuidhinisha kiongozi wa kundi la SELEKA, Michel Djotodia kuwa rais wa mpito wa nchi hiyo. Baraza hilo lenye wanachama 105 limemuidhinisha baada ya kukosekana mpinzani. Mwezi uliopita, Djotodia aliwaongoza waasi wa SELEKA kuipindua serikali ya Rais Francois Bozize ambaye kwa sasa anaishi uhamishoni nchini Benin.

Na Salum Bendera

Rais wa Somalia alaani mauaji ya Mogadishu


Rais wa Somalia alaani mauaji ya MogadishuRais Hassan Sheikh Mohamoud wa Somalia amelaani vikali mashambulio ya kigaidi ya jana katika mji mkuu Mogadishu na kusisitiza kwamba, mashambulio hayo yanaonesha kukata tamaa magaidi hasa baada ya kupoteza ngome zao zote. Rais wa Somalia amesisitiza kwamba, magaidi wamekata tamaa nchini humo hasa baada ya kushindwa kufikia malengo yao kufuatia kupoteza ngome zao zote na ndio maana wamekuwa wakitapata kwa kufanya mauaji ya kiholela nchini humo. Watu wasiopungua 34 waliuawa jana baada ya magari mawili yaliyotegwa mabomu kuripuka nje ya mahakama huko Mogadishu mji mkuu wa Somalia na baadae watu wenye silaha kulishambulia jengo la mahakama hizo kabla ya kuzuka mapigano ya silaha kati ya wavamizi hao na vikosi vya usalama vilivyokuwa vimelizingira eneo hilo. Wakati huo huo,

Sudan kuheshimu makubaliano na Sudan Kusini


Sudan kuheshimu makubaliano na Sudan KusiniMakamu wa Rais wa Sudan amesisitiza kuwa nchi yake inaheshimu na kusisitiza kutekelezwa makuablaino ya ushirikiano iliyofikia na jirani yake Sudan Kusini. Nafi Ali Nafi Makamu wa Rais Omar Hassan al Bashir wa Sudan amesisitiza kuwa Sudan itaheshimu kikamilifu makubaliano ya ushirikiano iliyosaini na serikali ya Sudan Kusini.
Makamu wa Rais wa Sudan ameyataja mashambulizi ya hivi karibuni katika mji wa Kadukali makao makuu ya mkoa wa Korofani Kusini kuwa ni njama za baadhi ya pande za kutaka kuvunja makubaliano hayo na kwamba mapatano hayo yataendelea kudumu licha ya njama hizo. Nafi Ali Nafi pia ameyataka makundi yote ya kisiasa ya Sudan kuungana na kujiweka mbali na maadui na kuongeza kuwa Sudan itaendelea kuijenga upya nchi hiyo ili kutimiza matarajio ya wananchi.

waliokamatwa na Silaha ni wahusika wakuu wa matukio ya kijambaza Z'bar


Jeshi la Polisi Zanzibar limefanikiwa kuwakamata watu wawili ambao wanasadikiwa kuwa ni mjambazi,waliokamatwa wakiwa na silaha ya SMG yenye risasi 29 ndani yake.


Akizungumza na waandishi wa habari huko Ofisini kwake makao makuu ya Jeshi la Polisi Zanzibar ziwani,Kamishna Mussa Ali Musaa aliwataja watu hao ambao ni Faustine Geogre miaka 36 Msukuma wa geita Ushirombo na Mohamed Ali Salum wa Bambuu Bububu.

Alisema kuwa awali Jeshi lake lilifanikiwa kumkamata Faustine wakati akiwa kwenye sehemu za starehe(baaar ya chuo cha mafunzo)ambae walimfanyia mahojiano na badae kumpekuwa na kumkuta akiwa na fedha za kigeni Dola za kimarekani 100,Naira za Nigeria 3540 na T,shs,370,000/= pamoja na simu 3 aina mbali mbali.

Kutokana na hatuwa hio ndipo Jeshi hilo badae likaamua kufanya upekuzi nyumbani kwa mtuhumiwa huyo na kumkuta na vitu vyengine kadhaa vikiwemo’’jeki 1 bisbisi 2 koleo la kukatia nyaya na baadhi ya vitu vyengine kadhaa”alisema kamishna Mussa.

Friday, April 12, 2013

Njama za Wazayuni dhidi ya al-Aqswa zaendelea


Njama za Wazayuni dhidi ya al-Aqswa zaendelea
Waziri wa Waqfu na Masuala ya Kidini wa serikali halali iliyochaguliwa na wananchi ya Palestina ametahadharisha kuhusiana na njama za utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Masjidul Aqswa. Ismail Ridhwan amesisitiza kwamba, msikiti mtakatifu wa al-Aqswa uko katika hatua hatari mno kutokana na hujuma na mipango ya kujitanua ya Israel sambamba na hatua zake za kuuyahudisha mji wa Baytul Muqaddas. Waziri wa Waqfu na Masuala ya Dini wa serikali ya Palestina inayoongozwa na Waziri Mkuu Ismail Hania amewataka Waislamu kote ulimwengu kukabiliana na njama hizo za utawala ghasibu wa Israe. Ismail Ridhwan amezitaka nchi za Kiislamu na Kiarabu, Jumuiya ya Nchi za Kiarabu, Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu OIC,

MSF: Wakimbizi wa Mali 74,000 wanahitajia msaada


MSF: Wakimbizi wa Mali 74,000 wanahitajia msaada Shirika la Madaktari Wasio na Mipaka (MSF) limetangaza kuwa, wakimbizi sabini na nne elfu wa Mali wanahitajia msaada wa haraka wa kibinaadamu. Taarifa ya shirika hilo imeeleza kuwa, wakimbizi wa Mali walioko nchini Mali wanakabiliwa na hali mbaya zaidi ya kibinaadamu na kwamba, wanahitajia misaada ya haraka ili waweze kukidhi mahitaji yao muhimu. Ripoti ya shirika hilo sambamba na kutoa wito wa kupelekewa misaada kwa wakimbizi hao wa Mali imeeleza kwamba, wakimbiz hao wanakabiliwa na uhaba pamoja na ukata wa huduma muhimu kama maji na chakula. Matatizo makubwa ya wakimbizi hao ni uhaba wa maeneo ya kujihifadhi, upungufu wa chakula, maji safi ya kunywa,

Mpalestina afa shahidi katika gereza la Israel


Mpalestina afa shahidi katika gereza la Israel
Mfungwa mwingine wa Kipalestina amekufa shahidi katika hali ya kutatanisha akiwa ndani ya gereza la kuogofya la Nafha huko Israel, Palestina inayokaliwa kwa mabavu.
Kufuatia kifo hicho, Wapalestina wanaoshikiliwa mateka katika magereza ya Utawala wa Kizayuni wa Israel waliitisha mgomo kwa lengo la kuwajuilisha walimwengu kuhusu hali yao mbaya inayowakabili. Mapema mwezi huu, Maisara Abu Hamdia,

CHADEMA yatishia kujiengua mchakato wa katiba TZ


Freeman Mbowe, Mwenyekiti Taifa wa CHADEMA na msemaji mkuu wa kambi ya upinzani katika Bunge la Tanzania
Chama cha Demokrasia na Maendeleo nchini Tanzania (Chadema), kimesema huenda kikachukua uamuzi mzito wa kujiengua kwenye mchakato wa kutafuta  katiba mpya  nchini humo iwapo mambo muhimu  na ya kimsingi hayatapatiwa ufumbuzi wake hadi ifikapo tarehe 30 Aprili mwaka huu. Taarifa iliyotolewa na chama hicho kikuu cha upinzani nchini Tanzania imeeleza kuwa, Chadema kinataka kufutwa uteuzi au uchaguzi wa wajumbe wa Mabaraza ya Wilaya ya Katiba uliofanywa na Kamati za Maendeleo za Kata na badala yake wajumbe wa Mabaraza ya Katiba ya Wilaya wachaguliwe moja kwa moja na wanachi wa Kata bila ya  kuchujwa na Kamati za Maendeleo za Kata. Wakati huohuo,

Adhana yaruhusiwa Sweden kwa mara ya kwanza


Adhana yaruhusiwa Sweden kwa mara ya kwanza
Msikiti mmoja katika kitongoji cha mji mkuu wa Sweden, Stockholm umeruhusiwa kuadhini kwa kutumia kipaza sauti kilicho kwenye mnara kwa ajili ya Sala ya Ijumaa. Hii ni mara kwa kwanza kwa nchi hiyo ya Scandinavia kuruhusu adhana kwa sauti inayosikika nje ya msikiti.
Idara ya polisi mjini Stockholm imesema msikiti huo utaruhusiwa kuadhini kwa muda wa kati ya dakika tatu na tano katika kipindi cha baina ya saa sita na saa saba mchana kila Ijumaa. Mkuu wa Jumuiya ya Utamaduni wa Kiislamu katika eneo la Botkyrka kusini mwa Stockholm Bw. Ismail Okur ameupongeza uamuzi huo. Ombi la kuadhini kwa sauti inayotoka nje ya msikiti liliwasilishwa miaka mitano iliyopita. Kuna karibu Waislamu 7,000 katika eneo hilo na aghalabu wana asili ya Uturuki. Chama chenye chuki dhidi ya Uislamu cha Sweden Democrats kimepinga uamuzi huo.

Tuesday, April 9, 2013

Chama cha Walimu Tanzania chaionya serikali


Chama cha Walimu Tanzania chaionya serikali Chama cha Walimu Tanzania (CWT), kimetaka Bunge na wazazi kuingilia kati uamuzi wa Serikali wa kukataa kukaa katika meza moja kwa ajili ya kuzungumzia nyongeza za mishahara na posho. Taarifa ya chama hicho imetahadharisha kuwa, vinginevyo Serikali inakaribisha mgomo mwingine wa walimu. Mwaka jana walimu nchini Tanzania waligoma kufanya kazi wakishinikiza nyongeza za mishahara, lakini Serikali ilikimbilia mahakamani. Aidha Mahakama ilisitisha mgomo huo kwa maelezo kuwa ulikuwa batili na baadaye, kuziagiza Serikali na CWT kukaa tena kwenye meza ya majadiliano. Rais wa Chama cha Walimu nchini Tanzania, Gratian Mukoba, amesema kuwa, pamoja na chama hicho kuwa tayari kuzungumza, Serikali ya Rais Kikwete imekataa kuzungumza nacho kuhusu nyongeza za mishahara na maslahi mengine ya walimu.

Njama ya nchi za Ghuba ya Uajemi kutangaza Hizbullah kuwa kundi la kigaidi


Njama ya nchi za Ghuba ya Uajemi kutangaza Hizbullah kuwa kundi la kigaidi
Spika wa Bunge nchini Bahrain, Khalifa bin Ahmed Al Dhahrani amefichua njama za Baraza la Ushirikiano la Ghuba ya Uajemi za kuiweka Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon katika orodha yake ya makundi ya kigaidi. Dhahrani amehoji juu ya uhusiano wa nchi yake na taifa la Lebanon endapo hatua hiyo itachukuliwa. Hata hivyo spika huyo wa bunge nchini Bahrain ametetea hatua hiyo kwa kudai kama ninavyo mnukuu, "Uhusiano na taifa la Lebanon hautabadilika kama ambavyo pia uhusiano kati ya nchi wanachama hautabadilika." Mwisho wa kunukuu. Ameongeza kuwa, wanachama wa Baraza la Ushirikiano ya Ghuba ya Uajemi wanalijadili kwa kina suala hilo. Kuhusiana na vizingiti vinavyozuia maelewano ya nchi wanachama wa baraza hilo Dhahrani amesema kuwa, kuna udharura wa nchi hizo kumaliza tofauti zao na kufikia maelewano.

Monday, April 8, 2013

Afrika Kusini kutuma wanajeshi Kongo DRC


Jeshi la Ulinzi wa Taifa la Afrika Kusini (SANDF) limesema kuwa litatuma wanajeshi wake huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kama sehemu ya kikosi cha Umoja wa Mataifa cha kusimamia usalama mashariki mwa nchi hiyo. Hayo yamesemwa leo na Brigedia Jenerali Xolani Mabanga wa Jeshi la Ulinzi wa Taifa la Afrika Kusini. Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wiki iliyopita lilipasisha azimio lilioidhinisha kutumwa kikosi cha uingiliaji kati huko Mashariki mwa Kongo ambapo serikali ya Afrika Kusini pia iliahidi kuchangia wanajeshi wake katika kikosi hicho.  Hata hivyo Brigedia Jenerali Mabanga amesema kuwa, bado haijafahamika tarehe ya

Azawad yasisitiza kujitawala kaskazini mwa Mali


Azawad yasisitiza kujitawala kaskazini mwa Mali
Harakati ya Ukombozi ya Azawad imetangaza kuwa, ingali inasisitiza juu ya mamlaka ya kujitawala eneo la kaskazini mwa Mali. Viongozi wa Harakati ya Azawad wamesisitiza juu ya kuweko mazungumzo yenye lengo la kupatikana amani na kuhitimishwa makumi ya miaka ya kukaliwa kwa mabavu eneo hilo na serikali kuu ya Mali. Msimamo huo wa Harakati ya Ukombozi wa Azawad ni jibu kwa ombi la Laurent Fabius Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Ufaransa aliyeitaka harakati hiyo iweke chini silaha na iingie katika mchakato wa kisiasa nchini Mali. Wakati huo huo, imeelezwa kuwa, hali ya kibinaadamu nchini Mali inazidi kuwa mbaya. Ripoti zinasema kuwa, watoto ndio wahanga wakuu wa mapigano na vita vya Mali. Mfuko wa Watoto wa Umoja wa Mataifa (UNICEF) umetangaza kuwa, watoto wanaokaribia laki mbili wanakabiliwa na hatari ya kufariki dunia au kujeruhiwa na milipuko ya mabomu nchini humo. UNICEF imesema kuwa mabomu hayo ambayo bado hayajalipuka yamesalia nchini Mali tangu mwanzoni mwa mapigano yanayoendelea sasa kati ya vikosi vya majeshi ya Ufaransa na makundi yenye silaha katike eneo la kaskazini mwa Mali.

Mafuriko yauwa watu tisa huko Luanda Angola


Mafuriko yauwa watu tisa huko Luanda Angola
Mafuriko yaliyoikumba Luanda mji mkuu wa Angola yameuwa watu wasiopungua tisa na wengine wanne hawajulikani walipo. Watu hao walipoteza maisha baada ya nyumba zao kubomolewa na mvua kali zilionyesha juzi huko Luanda mji mkuu wa Angola. Miongoni mwa wahanga wa mafuriko hayo ni watoto. Shirika la habari la utangazaji la Angola (Angop) limeripoti kuwa mafuriko hayo ya juzi yamebomoa mamia ya nyumba za raia na kusababisha hasara kubwa ya mali. Limesema nyumba 500 zimebomoka katika maeneo ya Samba na Coreia pekee mjini Luanda.

Thursday, April 4, 2013

DPP Zanzibar “Atupilia mbali uchunguzi mauwaji ya Padri Mushi”




Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) Zanzibar, Ibrahim Mzee Ibrahim, ametupilia mbali uchunguzi wa mauaji ya Padri Evarist Mushi uliofanywa na Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Maafisa wa Shirika la Upelelezi la Marekani (FBI) na kusema mtuhumiwa hana kesi ya kujibu mahakamani.


Padri Mushi ambaye alikuwa Paroko wa Kanisa Katoliki Minara Miwili aliuawa kwa kupigwa risasi Febuari 17, mwaka huu katika eneo la Beitrasi mjini hapa akiwa ndani ya gari alipokuwa akielekea kuongoza misa ya Jumapili katika Kanisa la Mtakatifu Theresia, mjini Zanzibar.

Baada ya mauaji hayo, Rais Jakaya Kikwete alitoa kibali cha kukaribisha maafisa wa FBI kushirikiana na Jeshi la Polisi kufanya uchunguzi wa mauaji hayo na Machi 17, mwaka huu Jeshi la Polisi lilimkamata Omar Mussa Makame kwa tuhuma za kuhusika na mauaji hayo.

Wasaudi milioni 10 hawana makaazi ya kudumu

Familia kubwa  Saudia inayoishi kwa umasikini katika makao duni
Uchunguzi uliofanywa hivi karibuni unaonyesha kuwa karibu raia milioni 10 wa Saudi Arabia ambao ni asilimia 60 ya raia wote nchini humo hawamiliki nyumba.
Gazeti la Al Watan la Saudi Arabia limesema nchi hiyo yenye utajiri mkubwa wa mafuta inakabiliwa na tatizo sugu la kuwajengea wananchi hasa vijana nyumba bora za kuishi.
Ripoti hiyo aidha imeongeza kuwa asilimia 20 ya Wasaudi wanamiliki nyumba lakini katika mitaa duni. Katika miaka ya hivi karibuni Saudi Arabia imekumbwa na uhaba mkubwa wa nyumba kutokana na waliochukua mikopo kuchelewa kuilipa pamoja na ongezeko kubwa la bei ya ardhi pamoja na sheria ngumu za benki.

Wednesday, April 3, 2013

Majasusi wa Uingereza walimuua Patrice Lumumba

Hayati Patrice Lumumba
Mbunge mmoja wa Uingereza amefichua kuwa Shirika la Kijasusi la Uingereza MI6 lilihusika katika mauaji ya Patrice Lumumba, waziri mkuu wa kwanza aliyechaguliwa kidemokrasia Kongo.
Lord David Edward Lea amefichua ukweli huo katika barua aliyoandikia jarida la London Review of Books toleo la Machi 21.
Edward Lea ambaye ni mjumbe katika Baraza la Malodi (House of Lords) amesema alidokezewa hayo na Daphne Park ambaye alikuwa jasusi na balozi mdogo huko mjini Leopoldville ambao sasa unajulikana kama Kinshasa kuanzia mwaka 1959 hadi 1961.

Shambulio la Taliban laua wa 44 Afghanistan


Wanamgambo wa Taliban nchini Afghanistan
Wanamgambo waasi waliokuwa wamevalia sare za jeshi la taifa la Afghanistan wameua watu 44 na kuwajeruhi wengine 100 baada ya kufanya shambulio dhidi ya majengo ya serikali katika jimbo la Farah. Gavana wa Jimbo la Farah Mohammad Akram Ekhpelwak amesema kuwa, kwa uchache washambuliaji wanane waliuawa kwenye shambulio hilo. Amesema kuwa, shambulio hilo lililofanywa na kundi la wanamgambo wa Taleban lilikuwa na lengo la kuwakomboa wapiganaji wenzao waliokuwa wamefikishwa mahakamani. Amesema kuwa, raia 34, wanajeshi sita na askari wanne wameuawa kwenye shambulio hilo. Ekhpelwak ameongeza kuwa, shambulio hilo lililenga majengo ya serikali zikiwemo ofisi ya mahakama na ile ya Mwanasheria Mkuu. 

Utata wa uchinjaji waibua machafuko Tanzania


Maafisa wa polisi wakiondoa vizuzi vilivyowekwa na waandamanaji, Tunduma, Tanzania 03 Aprili 2013 
Vurugu na ghasia zimeripotiwa kutokea nchini Tanzania katika mji wa Tunduma mkoani Mbeya, baada ya vijana kuandamana mitaani na kuchoma moto matairi ya magari  na kuweka vizuizi mabarabarani wakipinga hatua ya viongozi wa dini ya Kikristo katika eneo hilo la mpakani kumuandikia barua Mkuu wa Wilaya ya Momba wakitaka wapewe ruhusa ya kuchinja wakati wa sherehe za Pasaka.
Taarifa hiyo inaeleza kuwa, vijana wanaofanya kazi katika stendi ndio walioanzisha vurugu hizo majira ya asubuhi na kuvamiwa na jeshi la polisi lililotumia mabomu ya kutoa machozi ili kuwatawanya waandamanaji.