Spika wa Bunge nchini Bahrain, Khalifa bin Ahmed Al Dhahrani
amefichua njama za Baraza la Ushirikiano la Ghuba ya Uajemi za kuiweka
Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya Lebanon katika orodha
yake ya makundi ya kigaidi. Dhahrani amehoji juu ya uhusiano wa nchi
yake na taifa la Lebanon endapo hatua hiyo itachukuliwa. Hata hivyo
spika huyo wa bunge nchini Bahrain ametetea hatua hiyo kwa kudai kama
ninavyo mnukuu, "Uhusiano na taifa la Lebanon hautabadilika kama ambavyo
pia uhusiano kati ya nchi wanachama hautabadilika." Mwisho wa kunukuu.
Ameongeza kuwa, wanachama wa Baraza la Ushirikiano ya Ghuba ya Uajemi
wanalijadili kwa kina suala hilo. Kuhusiana na vizingiti vinavyozuia
maelewano ya nchi wanachama wa baraza hilo Dhahrani amesema kuwa, kuna
udharura wa nchi hizo kumaliza tofauti zao na kufikia maelewano.
Hii ni katika hali ambayo kwa mara kadhaa serikali ya Manama imekuwa ikitoa tuhuma zisizo na msingi wowote wala ushahidi kwamba, Harakati hiyo ya Hizbullah imekuwa ikichochea maandamano ya wananchi nchini Bahrain. Viongozi wa Hizbullah wamekuwa wakikanusha vikali madai hayo. Hatua hiyo inakuja huku hata Umoja wa Ulaya (EU) umekataa kuiweka harakati hiyo katika orodha ya makundi ya kigaidi na kusisitiza kuwa, Harakati ya Hizbullah ni chama kamili cha kisiasa ambacho hakifai kuitwa cha kigaidi.

No comments:
Post a Comment