Chama cha Walimu Tanzania (CWT), kimetaka Bunge na wazazi
kuingilia kati uamuzi wa Serikali wa kukataa kukaa katika meza moja kwa
ajili ya kuzungumzia nyongeza za mishahara na posho. Taarifa ya chama
hicho imetahadharisha kuwa, vinginevyo Serikali inakaribisha mgomo
mwingine wa walimu. Mwaka jana walimu nchini Tanzania waligoma kufanya
kazi wakishinikiza nyongeza za mishahara, lakini Serikali ilikimbilia
mahakamani. Aidha Mahakama ilisitisha mgomo huo kwa maelezo kuwa ulikuwa
batili na baadaye, kuziagiza Serikali na CWT kukaa tena kwenye meza ya
majadiliano. Rais wa Chama cha Walimu nchini Tanzania, Gratian Mukoba,
amesema kuwa, pamoja na chama hicho kuwa tayari kuzungumza, Serikali ya
Rais Kikwete imekataa kuzungumza nacho kuhusu nyongeza za mishahara na
maslahi mengine ya walimu.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment