Harakati ya Ukombozi ya Azawad imetangaza kuwa, ingali
inasisitiza juu ya mamlaka ya kujitawala eneo la kaskazini mwa Mali.
Viongozi wa Harakati ya Azawad wamesisitiza juu ya kuweko mazungumzo
yenye lengo la kupatikana amani na kuhitimishwa makumi ya miaka ya
kukaliwa kwa mabavu eneo hilo na serikali kuu ya Mali. Msimamo huo wa
Harakati ya Ukombozi wa Azawad ni jibu kwa ombi la Laurent Fabius Waziri
wa Mashauri ya Kigeni wa Ufaransa aliyeitaka harakati hiyo iweke chini
silaha na iingie katika mchakato wa kisiasa nchini Mali. Wakati huo huo,
imeelezwa kuwa, hali ya kibinaadamu nchini Mali inazidi kuwa mbaya.
Ripoti zinasema kuwa, watoto ndio wahanga wakuu wa mapigano na vita vya
Mali. Mfuko wa Watoto wa Umoja wa Mataifa (UNICEF) umetangaza kuwa,
watoto wanaokaribia laki mbili wanakabiliwa na hatari ya kufariki dunia
au kujeruhiwa na milipuko ya mabomu nchini humo. UNICEF imesema kuwa
mabomu hayo ambayo bado hayajalipuka yamesalia nchini Mali tangu
mwanzoni mwa mapigano yanayoendelea sasa kati ya vikosi vya majeshi ya
Ufaransa na makundi yenye silaha katike eneo la kaskazini mwa Mali.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment