Makamu wa Rais wa Sudan amesisitiza kuwa nchi yake inaheshimu na
kusisitiza kutekelezwa makuablaino ya ushirikiano iliyofikia na jirani
yake Sudan Kusini. Nafi Ali Nafi Makamu wa Rais Omar Hassan al Bashir wa
Sudan amesisitiza kuwa Sudan itaheshimu kikamilifu makubaliano ya
ushirikiano iliyosaini na serikali ya Sudan Kusini.
Makamu wa Rais wa Sudan ameyataja mashambulizi ya hivi karibuni katika mji wa Kadukali makao makuu ya mkoa wa Korofani Kusini kuwa ni njama za baadhi ya pande za kutaka kuvunja makubaliano hayo na kwamba mapatano hayo yataendelea kudumu licha ya njama hizo. Nafi Ali Nafi pia ameyataka makundi yote ya kisiasa ya Sudan kuungana na kujiweka mbali na maadui na kuongeza kuwa Sudan itaendelea kuijenga upya nchi hiyo ili kutimiza matarajio ya wananchi.

No comments:
Post a Comment