Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Monday, April 15, 2013

Rais wa Somalia alaani mauaji ya Mogadishu


Rais wa Somalia alaani mauaji ya MogadishuRais Hassan Sheikh Mohamoud wa Somalia amelaani vikali mashambulio ya kigaidi ya jana katika mji mkuu Mogadishu na kusisitiza kwamba, mashambulio hayo yanaonesha kukata tamaa magaidi hasa baada ya kupoteza ngome zao zote. Rais wa Somalia amesisitiza kwamba, magaidi wamekata tamaa nchini humo hasa baada ya kushindwa kufikia malengo yao kufuatia kupoteza ngome zao zote na ndio maana wamekuwa wakitapata kwa kufanya mauaji ya kiholela nchini humo. Watu wasiopungua 34 waliuawa jana baada ya magari mawili yaliyotegwa mabomu kuripuka nje ya mahakama huko Mogadishu mji mkuu wa Somalia na baadae watu wenye silaha kulishambulia jengo la mahakama hizo kabla ya kuzuka mapigano ya silaha kati ya wavamizi hao na vikosi vya usalama vilivyokuwa vimelizingira eneo hilo. Wakati huo huo,
kundi la wanamgambo wa Al-Shabab limetangaza kuhusika na mauaji ya jana mjini Mogadishu. Sheikh Ali Mohamud Rage, Msemaji wa wanamgambo wa Al-Shabab sambamba na kutangaza kuhusika kundi lao na mauaji hayo amesisitiza kwamba, mashambulio dhidi ya majengo na vituo vya serikali  nchini Somalia yataendelea.

Na Salum Bendera

No comments:

Post a Comment