Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Friday, April 12, 2013

MSF: Wakimbizi wa Mali 74,000 wanahitajia msaada


MSF: Wakimbizi wa Mali 74,000 wanahitajia msaada Shirika la Madaktari Wasio na Mipaka (MSF) limetangaza kuwa, wakimbizi sabini na nne elfu wa Mali wanahitajia msaada wa haraka wa kibinaadamu. Taarifa ya shirika hilo imeeleza kuwa, wakimbizi wa Mali walioko nchini Mali wanakabiliwa na hali mbaya zaidi ya kibinaadamu na kwamba, wanahitajia misaada ya haraka ili waweze kukidhi mahitaji yao muhimu. Ripoti ya shirika hilo sambamba na kutoa wito wa kupelekewa misaada kwa wakimbizi hao wa Mali imeeleza kwamba, wakimbiz hao wanakabiliwa na uhaba pamoja na ukata wa huduma muhimu kama maji na chakula. Matatizo makubwa ya wakimbizi hao ni uhaba wa maeneo ya kujihifadhi, upungufu wa chakula, maji safi ya kunywa,
madawa na matibabu, imebainisha taarifa ya shirika hilo la Madaktari Wasio na Mipaka (MSF). Hivi karibuni Mfuko wa Watoto wa Umoja wa Mataifa (UNICEF) ulitangaza kuwa, watoto wanaokaribia laki mbili wanakabiliwa na hatari ya kufariki dunia au kujeruhiwa na milipuko ya mabomu nchini Mali. UNICEF ilisema kuwa mabomu hayo ambayo bado hayajalipuka yamesalia nchini Mali tangu mwanzoni mwa mapigano yanayoendelea sasa kati ya vikosi vya majeshi ya Ufaransa na makundi yenye silaha katike eneo la kaskazini mwa Mali.

No comments:

Post a Comment