Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Sunday, April 21, 2013

Nigeria yaanzisha kampeni dhidi ya uvumi


Bango linalowaonyesha watu wakipashana uvumi na maandishi yanayo toa wito kwa Wanigeria 'kusema la kwa waeneza uvumi'
Wakuu wa jimbo lenye utajiri wa mafuta la Bayelsa nchini Nigeria wameanzisha kampeni maalamu yenye kauli mbiu ya 'sema la kwa waeneza uvumi'.
Kampeni hiyo imeanzishwa kufuatia kuibuka taharuki baada ya kuenea uvumi kuwa gavana wa jimbo hilo amefutwa kazi. Katika mabango yaliyowekwa barabarani Wanigeria wanahimizwa kutosikiliza uvumi wala kuuhimiza. Wanaoendesha kampeni hiyo wanasema uvumi umeathiri vibaya utendaji kazi katika jimbo hilo.
Msemaji wa gavana wa jimbo hilo Daniel Iworiso-Markson amewaambia waandishi habari kuwa kampeni hiyo haina lengo la kuwanyima watu uhuru wa maoni. Ili kukabiliana na tatizo la uvumi katika jamii, wakuu wa jimbo hilo wamebuni kamati ya wataalamu watakaowaelimisha watu kuhusu uovu wa kueneza uvumi. Aidha serikali ya jimbo hilo imetangaza nambari maalumu za simu ili kila mwenye kutaka habari rasmi azipate kupitia njia hiyo badala ya kutegemea uvumi. Jimbo la Bayelsa ni nyumbani kwa Rais Goodluck Jonathan wa Nigeria.

No comments:

Post a Comment