Mfungwa mwingine wa
Kipalestina amekufa shahidi katika hali ya kutatanisha akiwa ndani ya
gereza la kuogofya la Nafha huko Israel, Palestina inayokaliwa kwa
mabavu.
Kufuatia kifo hicho,
Wapalestina wanaoshikiliwa mateka katika magereza ya Utawala wa Kizayuni
wa Israel waliitisha mgomo kwa lengo la kuwajuilisha walimwengu kuhusu
hali yao mbaya inayowakabili. Mapema mwezi huu, Maisara Abu Hamdia,
mfungwa mwingine wa Kipalestina alikufa shahidi akiwa ndani ya gereza
huko Israel. Mateka wapatao elfu 5 wa Kipalestina wanashikiliwa katika
jela za utawala haramu na ghasibu wa Israel. Utawala huo ghasibu
unaendelea kutekeleza siasa zake za kimabavu dhidi ya Wapalestina kwa
kuwaua na kuwakandamiza raia wasiokuwa na hatia yoyote. Tangu mwaka 1948
hadi hii leo, zaidi ya Wapalestina laki nane na nusu wamekamatwa na
kuswekwa katika jela za kutisha za utawala wa Kizayuni. Kuendelea hatua
za ukandamizaji za utawala wa Kizayuni dhidi ya mateka wa Kipalestina na
udhaifu wa jumuiya za kimataifa katika kufuatilia faili la mateka hao
kumezidisha machungu ya wananchi wanaokandamizwa wa Palestina. Hii ni
katika hali ambayo jamii ya kimataifa imeendelea kunyamazia jinai za
utawala haramu wa Israel, sambamba na utawala huo ghasibu kuungwa mkono
na kusaidiwa na nchi za Magharibi.
No comments:
Post a Comment