Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu OIC imetoa wito wa kutumwa
kamati ya jumuiya hiyo nchini Myanmar kwa shabaha ya kushuhudia kwa
karibu hali inayowakabili Waislamu wa jamii ya Rohingya wa nchi hiyo.
Taarifa ya mwisho ya mkutano wa kamati ya mawasiliano ya OIC imeitaka
serikali ya Myanmar kuruhusu kamati ya mawaziri ya jumuiya hiyo kutumwa
katika nchi hiyo. Akizungumza katika mkutano huo, Profesa Ekmeleddin
İhsanoğluKatibu Mkuu wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu OIC amesema
kuwa, utumiaji mabavu unaofanywa dhidi ya Waislamu wa Myanmar
haukubaliki hata kidogo na kwamba, hiyo ni ishara ya utendaji mbaya wa
serikali ya nchi hiyo. Ni mwaka mmoja sasa ambapo OIC imekuwa ikitaka
kutuma kamati ya uchunguzi nchini Myanmar lakini bado haijafanikiwa hadi
sasa. Katika taarifa yake, Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu OIC
imeitaka Kamisheni ya Haki za Binadamu ya Umoja wa Mataifa kutuma timu
ya uchunguzi nchini Myanmar. Aidha OIC imezitaka nchi jirani na Myanmar
kama Bangladesh na Malaysia kusaidia kutatua tatizo la Waislamu wa
Rohingya wanaoandamwa na wimbi la mauaji yanayofanywa na Mabudha wenye
misimamo mikali wakishirikiana na askari wa jeshi la serikali ya
Myanmar.
Na Salum Bendera
Na Salum Bendera
No comments:
Post a Comment