Vurugu na ghasia zimeripotiwa kutokea nchini Tanzania
katika mji wa Tunduma mkoani Mbeya, baada ya vijana kuandamana mitaani
na kuchoma moto matairi ya magari na kuweka vizuizi mabarabarani
wakipinga hatua ya viongozi wa dini ya Kikristo katika eneo hilo la
mpakani kumuandikia barua Mkuu wa Wilaya ya Momba wakitaka wapewe ruhusa
ya kuchinja wakati wa sherehe za Pasaka.
Taarifa hiyo inaeleza kuwa, vijana wanaofanya kazi katika
stendi ndio walioanzisha vurugu hizo majira ya asubuhi na kuvamiwa na
jeshi la polisi lililotumia mabomu ya kutoa machozi ili kuwatawanya
waandamanaji.
Hivi karibuni kulitokea machafuko na hata baadhi ya watu
kuuawa na kujeruhiwa nchini Tanzania, baada ya Wakristo kutaka wachinje
wanyama badalada ya Waislamu, jambo ambalo linapingwa na serikali na
Waislamu. Waziri Mkuu wa Tanzania Mizengo Pinda alinukuliwa akisema
kuwa, utamaduni uliozoeleka nchini humo ni kwa Waislamu kuchinja nyama
zinazouzwa mabuchani.
No comments:
Post a Comment