Waziri wa Waqfu na Masuala ya Kidini wa serikali halali
iliyochaguliwa na wananchi ya Palestina ametahadharisha kuhusiana na
njama za utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya Masjidul Aqswa. Ismail
Ridhwan amesisitiza kwamba, msikiti mtakatifu wa al-Aqswa uko katika
hatua hatari mno kutokana na hujuma na mipango ya kujitanua ya Israel
sambamba na hatua zake za kuuyahudisha mji wa Baytul Muqaddas. Waziri wa
Waqfu na Masuala ya Dini wa serikali ya Palestina inayoongozwa na
Waziri Mkuu Ismail Hania amewataka Waislamu kote ulimwengu kukabiliana
na njama hizo za utawala ghasibu wa Israe. Ismail Ridhwan amezitaka nchi
za Kiislamu na Kiarabu, Jumuiya ya Nchi za Kiarabu, Jumuiya ya
Ushirikiano wa Kiislamu OIC,
asasi za Kiislamu na maulama kwa ujumla
kutekeleza majukumu yao ipasavyo na hivyo kusimama na kutetea matukufu
ya Kiislamu. Ikumbukwe kuwa, mji wa Quds na msikiti mtakatifu wa
al-Aqswa vimekuwa vikikabiliwa na njama za kila leo tangu utawala bandia
wa Israel uasisiwe katika ardhi za Palestina miongo sita iliyopita.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment