Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Sunday, December 28, 2014

MISRI NA MOROCCO ZAPIGA MARUFUKU FILAMU INAYOMUONESHA MUNGU

Misri na Morocco zimepiga marufuku filamu iliyotengenezwa Hollywood isioneshwe katika mataifa hayo ya Afrika Kaskazini. Vyombo vya habari nchini Morocco vimetangaza kuwa mameneja wa sinema katika pembe zote za nchi hiyo wamepewa maagizo ya kutoonesha filamu iliyojaa utata ya “Exodus: Gods and Kings,” kwa sababu “inamuonesha Mungu,” jambo ambalo ni haramu katika Uislamu. Mapema waziri wa utamaduni wa Misri, Gaber Asfour alisema kuwa filamu hiyo imejaa makosa lukuki ikiwa ni pamoja na madai kwamba “[Nabii] Mussa na Wayahudi ndio waliojenga mapiramidi,” na kuongeza kuwa, “hilo linapingana kabisa na taaarifa za kihistoria zilizothibitishwa”. Adiha, waziri huyo ameashiria kuwa filamu hiyo iliyoongozwa na Ridley Scott, ni ya kizayuni na imetengenezwa kwa malengo ya kisiasa. “Inatoa historia kwa mujibu wa uzayuni na ina makosa lukuki ya kihistoria na ndio maana tumeamua kuipiga marufuku”, alisema. Mapema mwezi Mei, mwandishi na mtunzi maarufu wa filamu Art Olivier alisema kuwa makampuni mengi ya filamu za Hollywood zinamilikiwa na wafanyabishara wa Kizayuni. Kwa miaka kadhaa Hollywood imekuwa ikitengeneza filamu nyingi zinazolenga kuuchafua Uislamu na Waislamu.

Saturday, December 27, 2014

MAASKOFU WAMPONGEZA RAIS KIKWETE



dar-es-salaam.

maaskofu wa madhehebu mbalimbali za kikristo nchini wamepongeza uamuzi wa rais wa jamhuri ya muungano wa tanzania  dr jakaya mrisho  kikwete wa kuwawajibisha watendaji  wake.
wakizungumza kwa mnasaba wa sikukuu ya krismasi maaskofu hao, wametaka  kutoishia kuchukua hatua  kwa  waliotajwa kuhusika na sakata la akaunti ya tegeta escrow pekee, bali  kuwachukulia hatua wazembe  na wote wanaokutwa na tuhuma mbalimbali katika utawala wake.
naye askofu michael hafidh wa zanzibar  amemshauri rais kikwete  kuendeleza utaratibu wa kuwawajibisha viongozi wazembe na wasio waadilifu katika  kazi  zao.

BALOZI SEIF AZURU MSIKITI MKONGWE AFRIKA MASHARIKI



ZANZIBAR.
MAKAMU WA PILI WA RAIS WA ZANZIBAR  AL-HAJJ BALOZI SEIF ALI IDDI AMETEMBELEA MSIKITI MKONGWE ZAIDI KATIKA  UKANDA WA AFRIKA MASHARIKI ULIOPO MICHEWENI MKOA WA KASKAZINI PEMBA.
AKISALIMIANA NA UONGOZI WA KAMATI YA MSIKITI HUO PAMOJA NA BAADHI YA WAANZILISHI  WAKE,  BALOZI SEIF ALIWAKUMBUSHA WAUMINI WA DINI YA KIISLAMU KUENDELEA KUSHIKAMANA KAMA MAAMRISHO YA DINI YAO YANAVYOELEKEZA.
AMESEMA KUWA DINI YA KIISLAMU IMEKUWA  IKISISITIZA SUALA LA AMANI, JAMBO AMBALO LITAKAPOFUATWA NA KUTEKELEZWA IPASAVYO  HUSAIDIA KUWAPA UTULIVU  WANANCHI  KUFANYA IBADA NA SHUGHULI  ZAO  KAMA  KAWAIDA.
AIDHA  BALOZI SEIF AMEWAASA WAISLAM KUWA MAKINI KATIKA KUCHANGANYA DINI NA SIASA KAMA BAADHI YA WATU  HUSUSAN WANASIASA KUJARIBU KUSHAWISHI WATU KUFANYA HIVYO, MATOKEO YAKE NI KUANZISHA CHECHE ZA UHASAMA NA WASI WASI KATIKA JAMII.
MSIKITI WA IJUMAA WA MICHEWENI MJINI UNAKISIWA KUJENGWA TOKEA KARNE YA 14, KIPINDI AMBACHO KILIKUWA NA HARAKATI ZA KUSAMBAZWA  KWA DINI YA KIISLAMU KATIKA MWAMBAO WA AFRIKA MASHARIKI.