1- Kula au kunywa kwa kukusudia.
2- Kila kinachoingia tumboni au kooni kwa kukusudia.
3- Kukutana kimwili (kuingiliana) kati ya mume na mke.
4-
Kujitoa manii (mbegu za uzazi) au kusababisha kutokwa na manii (kwa
kujichezea sehemu za siri, kukumbatiana au kupigana mabusu nakadhalika).
5-
Kujitapisha kwa makusudi. Imepokewa hadithi kutoka kwa Abu Hurayrah
(radhiya Allahu 'anhu) amesema: amesema Mtume (Swalla Allahu 'alayhi wa
sallam): {...na mwenye kujitapisha basi inamuwajibikia kulipa.}
(wameipokea maimamu watano).
6- Kutokwa na damu ya mwezi (hedhi) au damu ya uzazi (nifasi).
*Wakati
wowote yanapomtokea mwanamke mawili hayo funga yake ya siku hio itakuwa
imeharibika na itamlazimikia kuilipa siku hio baada ya mwezi wa
Ramadhani.
No comments:
Post a Comment