Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Thursday, July 5, 2012

MATATIZA YA ZANZIBAR YANATOKANA NA WAZANZIBAR WENYEWE

Najua kama kukanusha ndio tabia ya binaadamu kwani aambiwae ukweli huwa si rahisi kuukubali ukweli huo kama viongozi wa zanzibar ndio chimbuko la migogoro yote yanayojitokeza katika muungano.
Wamezoeya kupiga kofi japo kwamba jambo linawakandamiza ilimradi posho inaingia mifukoni mwao ni muhali kulipinga.
Leo tumefika hapa waliorithi wapiga kofi nao sasa wanajaribu kutaka kukanusha lakini wapi ,farasi ameshakimbia ndio tamko linatoka “funga banda funga banda’ iko haja gani ya kufunga banda huku wakilaumiana kisiri siri .
Mwalimu nyerere katika mkutano wake mmoja nakumbuka alisema”wazanzibari tunawabembeleza angalau waseme jambo katika vikao lakini hakuna anaesema ,basi nyinyi wazanzibari hamna shida na hapa katika kikao ndipo pa kusema matatizo yenu?”
Wazanzibari wakiwa bungeni hawajui kusema ni mabubu lakini wakirudi nyumbani zanzibar ni mahodari kupanga mbinu za kuwadhoufisha wananchi,sasa tusemeje ?si ndio wao wenye matatizo?.
Kadhia hii haitaisha kwa wazanzibari matapeli ,ni mahodari kuomba ridhaa za wazanzibari lakini wakeshapewa huwa wadodosaji wakubwa katika bunge na hata wawakilishi.
Lengine ni kwamba wanaojichukulia ridhaa kwa nguvu ,wizi na hadaa kutoka kwa wananchi huwa si watu wema,wasomi au wenye kujua jambo ila ukereketwa ambao hautaisaidia zanzibar kuendelea mbele ila kurudi nyuma nyuma nyuma mpaka tugubikwe na kiza na kweli giza limeshatugubika.
Sidhani kama tunaweza kuondokana na aina hii ya wapiga kofi,wasinzilizi mpaka kuangukwa na udenda kikaoni,wachochezi wa kudhoufisha na kuwakandamiza wananchi wa chini hata ikibidi kuwapandikizia kesi zisizo kichwa wala miguu.alimradi dhulma juu ya dhulma nasi hatutambui na hatutatambua mpaka laana na ghadhabu za Mola wetu zitumalize ,yote ni nani ? ni wazanzibari wenyewe.
Tusipate taabu ya kumtafuta mchawi ,wachawi ni sisi wenyewe wazanzibari na hatutafika pahali mpaka wachawi wote wadhibitiwe na allah na inshaalla atawadhibiti.
Wachawi wengi wameshapita na hawa tulionao sasa inshaalla Mola atawadhibiti kisha atuangazie nuru itokayo kwake kwa umoja wetu wazanzibari.
Tumebaki kuwasifu ,kiongozi huyu hodari,kiongozi huyu hivi ,hakuna hata mmoja wote wachawi wa nafsi nyingine .
Kama ni kweli viongozi wazuri wangeliagiza wananchi wapigwe mabomu kama yaliyotokezea mahonda na donge? ila matatizo ni wazanzibari wenyewe ,hata kama serikali ya tanzania imetoa agizo hilo ,ina mamlaka gani ndani ya zanzibar ikiwa viongozi wa zanzibari wenyewe hawataki

No comments:

Post a Comment