Lakini Naibu Kiongozi wa Uamsho, Hamdan alikanusha jumuiya yake kuhusika na vurugu hizo akisema walikuwa msikitini kuwaombea dua waliofikwa na maafa katika meli ya MV Skaget Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mjini Magharibi, Azizi Juma Mohamed alisema jana kuwa viongozi hao wanatafutwa kwa kosa la kuwahamasisha vijana kufanya vurugu na kusababisha uharibifu wa miundombinu.
Alisema katika vurugu hizo, vijana hao walikata miti iliyomo pembeni mwa barabara, kuvunja vioo vya nyumba na magari , kuweka mawe na vitu vizito barabarani. Kamanda alisema viongozi hao waliomba kibali cha kufanya mikutano kwenye uwanja wa mzalendo ili kuwaombea dua waliokufa kwa ajali ya meli ya Mv Skagit lakini polisi ilikataa kutokana na amri ya serikali kuzuia mihadhara.
Kamanda Azizi alisema kwa kuwa kundi hilo la Uamsho linafahamika kwa ubishi ndipo jeshi hilo lilipeleka polisi kwenye uwanja wa Mzalendo ili kuzuia mkusanyiko wa wafuasi hao wa Umsho.
“Polisi waliwahi kuwazuia wafuasi hao wasikusanyike kwenye viwanja hivyo lakini viongozi wa Uamsho waliwatangazia wafuasi wao wakiwataka sasa wakusanyike kwenye viwanja vya msikiti wa Mbuyuni karibu na eneo la Malindi,” alisema Kamanda.
Alisema muda wa kuomba dua ulipofika viongozi hao waliingia msikitini lakini watu wengi zaidi walikuwa nje ya msikiti huo.
Kamanda alisema kilichoendelea kwenye msikiti huo ni viongozi huo ni kwa viongozi hao kukashfu viongozi wa serikali na kuwataka wafuasi wao kutounga mkono muungano.
Alisema wakati hayo wakiendelea,wafuasi wa Uamsho wakiwa na bendera walianza vurugu kupanga mawe barabarani na kuchoma moto matairi. Alisema ndipo Jeshi la Polisi likaamua kutumia nguvu kuwatawanya kwa mabomu ya machozi na maji yenye kemikali za kuwasha.
Akijibu tuhuma hizo, Naibu Kiongozi huyo wa Uamsho, Hamdan vurugu hizo zimesababishwa na polisi wenyewe kwani wao walikuwa msikitini wakiomba dua waliofikwa na maafa ya ajali ya Mv Skaget.
“ Tunasikitika sana viongozi wa dini kuhusishwa na vurugu zilizotokea jana (juzi), kwa kweli sisi hatuhusiki na vurugu hizo na tumeshangazwa na Jeshi la Polisi kuvamia msikitini na kuanza kuwatawanya waumini waliokuwa wakifanya ibada,” alisema.
Alisema baada ya sala hiyo walitoa mawaidha ya kuwataka waumini wao wasiilaumu serikali katika tukio la ajali na wachukulie kwamba huo ni mtihani kutoka kwa Mungu. Hamdani alisema hata kama vijana hao walibeba bendera za Uamsho wao lakini hawana uhusiano wowote na jumuiya yao.
“Bendera ni kitambaa ambacho mtu yoyote anaweza kuwa nacho na isichukuliwe kila mwenye bendera ya Uamsho ni mwanachama wa jumuiya hiyo,” alisema
Alishangazwa na Jeshi la Polisi kutumia nguvu kubwa kwa kurusha mabomu hadi mitaani hasa katika kipindi hiki ambacho watanzania wanaomboleza vifo vya ndugu na jamaa zao waliopotea katika ajali ya meli.
No comments:
Post a Comment