Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Tuesday, July 24, 2012

Madrasatul Twariqatul Irshaad inahitaji Swadaqatun Jaariyah Ramadhaan hii


 Hii ni sehemu ya moja ya Madarasa yanayohitajia kukamilishwa
 Sehemu ya nje ya moja ya Madarasa ya Madrasatul Twariiqatul Irshaad
 Sehemu wanazosomea wanafunzi

 Sehemu ya jengo linalosubiri Sadaka na msaada wako liweze kumalizika InshaaAllaah
Sehemu ya kisima kinachowapatia mahitajio ya maji.


Madrasatul Twariiqatul Irshaad ipo Tunguu maarufu kwa Shemego wilaya ya kati katika kisiwa cha Unguja.

Hivi sasa ina takriban wanafunzi zaidi ya 350 ambao wanaingia kwa mikupuo miwili asubuhi na jioni.

Ni moja katika Madrasah zilizopiga hatua kubwa katika kuwasomesha watoto Qur’aan pamoja na masomo ya dini. Kila mwaka inatoa wanafunzi wanaoshiriki mashindano ya kuhifadhi Qur’aan ya kitaifa.

Kwa kuongezeka wanafunzi wa ziada imeamua kuongeza sehemu za majengo yake kuweza kukabiliana na ongezeko la wanafunzi wamekwama kidogo wanataka kukwamuliwa.  Wanahitajia sadaka zenu, misaada yenu ya hali na mali katika kufanikisha azma yao hii. Wanaomba pia du’aa zenu Ramadhaan hii Mola awawafikishe katika kumaliza jengo lao.


Tukumbuke hadithi ya Mtume Swalla Allaahu ‘Alayhi Wasallam “ Mbora wenu ni Yule mwenye kujifunza Qur’aan kisha akaifundisha”

Pia tukumbuke hadithi nyengine ya Mtume Swalla Allaahu ‘Alayhi Wasallam aliposema “ Haitopungua mali ya mja kwa kutoa Sadaka”

Hii ni fursa ya kuiambatanisha funga yako ya Ramadhaan mwaka huu na Sadaka yenye kuendelea (Swadaqatun Jaariyah) kwa kuisaidia Madrasatul Twariiqatul Irshaad ya Tunguu kwa chochote utakachojaaliwa ili iweze kukamilisha majengo yaliyobakia. 

Misaada ya aina yoyote inakaribishwa na yote itatumika katika malengo yaliyokusudiwa

Kwa maelezo zaidi na wapi kuifikisha Misaada, wasiliana na Mudiyr               ( Mwalimu Mkuu) wa Madrasah, Maalim Juma 0777202790

Wabillaahi Attawfiyq – Ramadhaan Mubaarak

No comments:

Post a Comment