Nyudhuru za kuacha kufunga zinatofautiana na kila udhuru una hukumu yake, na hapa nitazielezea nyudhuru hizo kwa ufupi.
1- Hedhi
(damu ya mwezi) na nifasi (damu ya uzazi), huu ni udhuru ambao
unamlazimisha mwanamke kuacha kufunga, na inakuwa haramu kwake funga na
iwapo atafunga haitosihi
2-
(haitokubaliwa) funga yake, na ni wajibu kwake kulipa funga hiyo.
2-
Maradhi au Safari. Na mwenye udhuru wa maradhi (yanayotibika kwa
kawaida) pamoja na msafiri wanaruhusiwa kutokufunga na itawawajibikia
kulipa. Amesema Allah (Subhaanahu wa Ta'ala) :{{Atakaye
kuwa katika mji katika huu mwezi (wa Ramadhani) afunge. Na mwenye kuwa
mgonjwa au safarini, basi (atimize) hisabu (ya siku alizoacha kufunga)
katika siku nyingine. Mwenyezi Mungu anakutakieni yaliyo mepesi wala
hakutakieni yaliyo mazito.. .}} (2:185). Na kama maradhi yatazidi au kumletea madhara iwapo atafunga basi itakuwa lazima kwake kutokufunga.
*Ama
safari ambayo inaruhusiwa kwa sababu yake kutokufunga wanachuoni wengi
wemesema: Ni safari ya siku mbili kwa ngamia au kwa mwendo wa miguu
(mar-hala mbili) ambayo ni sawa na umbali wa takiribani kilomita (85km).
Na ruhusa hii inapatikana kwa msafiri anayesafiri kwa chombo cha aina
yoyote atakachosafiria,ijapo kwa dhahiri safari hiyo haimpi uzito
wowote.
3-
Vizee (vikongwe) na wenye maradhi sugu (yasiotarajiwa kupoa). Na haya
mawili iwapo yana msababishia madhara basi ni katika udhuru na ruhusa ya
kuacha kufunga, na itamlazimikia atoe fidia kwa kumlisha masikini
kibaba (mudi) cha chakula (ambacho ni sawa na na uzito wa gramu 600g takiribani)au chakula kinacho mshibisha masikini mmoja kwa kila siku aliyoacha kufunga.
4- Waja wazito na wanyonyeshaji.
Nao ni katika wenye ruhusa ya kutokufunga, na inawabidi kulipa siku walizoshindwa kufunga kwa sababu ya udhuru huo.
No comments:
Post a Comment