Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Wednesday, October 30, 2013

KIKUNDI KINGINE CHA KIGAIDI CHAIBULIWA MSITUNI HUKO MKOANI TANGA....WALIKUWA NA BUNDUKI TATU, MAPANGA 18 NA VISU..!!


Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Luteni mstaafu Chiku Gallawa, amesema watu waliomuua askari mgambo Salum Mgonje na kumpiga risasi Mkuu wa Kituo cha Polisi Songe, wilayani Kilindi Edward Lusekolo ni kikundi kilichokuwa kinaishi msituni.

Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Luteni mstaafu Chiku Gallawa

  Alisema kikundi hicho kinaipinga Serikali ya Rais Jakaya Kikwete na kudai ni ya kikafiri kikiwa na mipango ya kutaka Tanzania isitawalike.Akizungumza na waandishi wa habari Mjini Handeni, Bi. Gallawa alisema kikundi hicho kiliweka kambi tatu wilayani humo kikifanya mafunzo mbalimbali yakiwemo ya kijeshi.
“Pia kikundi hiki ndicho kilichokuwa kikipinga mchakato wa sensa mwaka 2012, kambi zao tatu zilikuwa katika Kata ya Lwande na Negero kwenye Kijiji cha Madina.“Katika kambi ya Madina, wafuasi wao wawili wameuawa baada ya kupinga kitendo cha kukamatwa na askari Oktoba 26 mwaka huu wakijiita wafuasi wa Sunni,” alisema.
Aliwataja wafuasi waliouawa kuwa ni Ramadhan Hamis, ambaye ni mfanyabiashara wa madini na mwingine jina lake halikufahamika mara moja lakini inasemekana ni mwalimu wa dini ya Kiislamu (ustaadh) Kijiji cha Lwande.

Aliongeza kuwa, kikundi hicho kimekutwa na bunduki tatu aina ya gobore, shortgun moja, bastola mbili zilizotengenezwa kienyeji, mapanga 18 na visu 10.  Bi. Gallawa alisema wafuasi 46 wa kikundi hicho tayari wamekamatwa lakini jambo la kushangaza wamo watumishi wa Serikali ambao ni walimu wa shule za msingi na watafikishwa mahakamani wakati wowote. 
 
Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa, ambayo inaongozwa na Bi. Gallawa, imeamua kuweka kambi Kilindi kwani hivi sasa hali ya usalama si nzuri hadi itakapotulia. Akizungumza na Majira hivi karibuni, Kamanda wa Polisi mkoani humo, Constantine Masawe, alisema askari mgambo Salum Mgonje aliuawa Oktoba 22 mwaka huu ambapo Edward alipigwa risasi za mbavu na mkononi Oktoba 23, saa mbili usiku. 
 
Kikundi hicho kinajumuisha wakazi wa vijiji mbalimbali wilayani humo ambao wamefukuzwa na wenzao kutokana na tabia zao za kupinga mambo mbalimbali ya maendeleo. Chanzo cha kuanzishwa kikundi hicho ni baada ya mwenzao mmoja ambaye ni mfanyabiashara kutakiwa kulipa ushuru katika Kijiji cha Lwande na kukataa hivyo mgambo waliingilia kati ndipo wafuasi wao walichukua uamuzi wa kwenda kuwakata mapanga mgambo ambao mmoja alijeruhiwa na mwingine kuuawa.


----MAJIRA

Wataka sheria ya maandamano irekebishwe Misri


Wataka sheria ya maandamano irekebishwe MisriKituo cha kitaifa cha kutetea haki za biandamu cha Misri kimetaka sheria inayohusu maandamano ifanyiwe marekebisho. Kituo hicho kimeeeleza kuwa, katika rasimu ya katiba kuna baadhi ya vipengee vinavyobana haki ya wananchi ya kuandamana kwa amani. Kituo hicho cha kutetea haki za binadamu cha Misri kimesema, utangulizi wa katiba unapaswa kutambua haki isiyopingika ya kuandamana wananchi, na kwamba wananchi wanaweza kueleza malalamiko yao bila kizuizi chchote kwa maandamano ya amani.
Sheria ya maandamano katika rasimu ya katiba ya Misri inaeleza kuwa, ni marufuku waandamanaji kukaribia maeneo ya serikali na kidiplomasia, maafisa wa usalama wanapaswa kuarifiwa juu ya maandamano kabla ya maasaa 24 na hakuna haki ya kukusanyika katika meidani na kufunga barabara.

Israel yawaachia huru mateka 26 wa Palestina


Israel yawaachia huru mateka 26 wa PalestinaUtawala wa Kizayuni wa Israel umewaachilia huru mateka 26 wa Palestina, kama sehemu ya makubaliano ya kuanza tena mazungumzo eti ya amani  ya Mamlaka ya Ndani ya Palestina. Sivan Weizman msemaji wa jela za Israel ameeleza kuwa, 21 kati ya mateka hao walioachiliwa huru ni wa Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na watano kati yao wanatoka Ukanda wa Gaza. Mateka 104 wa Palestina wanatarajiwa kuachiliwa huru  miezi ijayo kutoka katika jela za kuogofya za utawala ghasibu wa Israel.
Nderemo na vifijo vilizikika kuanzia leo asubuhi wakati familia na viongozi wa Kipalestina katika Ukingo wa Magharibi na Ukanda wa Gaza walipokuwa wakiwapokea mateka hao walioachiliwa huru na Israel.
Hata hivyo mazungumzo hayo eti ya  kusaka amani kati ya Tel Aviv na Mamlaka ya Ndani ya Palestina yanapingwa na wananchi wengi na makundi ya mapambano ya Palestina.

Tuesday, October 29, 2013

NDEGE YA MAREKANI ISIYOENDESHWA NA RUBANI YAMTUNGUA KIONGOZI WA NGAZI YA JUU WA KUNDI LA AL-SHABAAB NA KUMUA NCHINI SOMALIA.

http://images2.wikia.nocookie.net/__cb20130713210228/uzbrojenie/pl/images/f/fb/Air_uav_mq-1_predator_lg.jpg

KIONGOZI wa ngazi ya juu anayeongoza mashambulizi ya kujitoa mhanga ya kundi la al-Shabaab lenye mafungamano na al-Qaeda ameuawa katika shambulizi la ndege isiyor
uka na rubani Kusini mwa Somalia
Waziri wa Mambo ya Ndani, Abdikarin Hussein Guled, ameiambia redio ya serikali kuwa idara ya ujasusi ilikuwa ikimfuatilia Ibrahim Ali Abdi, maarufu kama Anta-Anta, kwa muda sasa kabla ya shambulizi hilo kufanywa jana Jumatatu.


Waziri huyo hajasema ni nani aliyefanya shambulizi hilo, lakini afisa mmoja mjini Washington amesema jeshi la Marekani lilifanya shambulizi la ndege isiyoruka na rubani likililenga kundi la al-Shabaab nchini Somalia jana Jumatatu.


"Operesheni hiyo ambayo mtu huyu aliuawa ilikuwa muhimu kwa serikali. Mtu huyu alikuwa na jukumu kubwa kwa raia wengi wasio na hatia na kifo chake kitasaidia kurejesha amani," alisema waziri huyo kupitia Radio Mogadishu.
 
Maafisa kutoka serikali ya Somalia inayoungwa mkono na jamii ya kimataifa wamemtaja mwanamgambo aliyeuawa kuwa anayefahamika vyema kwa kutengeneza mabomu ya kuvaa mwilini pamoja na ya kutengwa ndani ya gari ambayo hutumiwa mara kwa mara na waasi kuyashambulia maeneo ya serikali. Hapajakuwa na kauli yoyote kutoka kwa wapiganaji hao.


Shambulizi hilo linakuja wiki chache baada ya shambulizi kali kufanywa katika jumba la maduka ya Westgate jijini Nairobi, Kenya, lililodaiwa kufanywa na al-Shabaab ambapo watu 67 waliuawa.


Kisha kikosi maalumu cha jeshi la wanamaji la Marekani kikafanya shambulizi katika bandari ya kusini ya Barawe mapema mwezi huu (Oktoba) na kushindwa kufikia lengo lake: ambalo lilikuwa ni kiongozi mmoja wa ngazi ya juu wa al-Shabaab na Mkenya mwenye asili ya kisomali kwa jina Abdulkadir Mohammed Abdulkadir, pia anayefahamika kama Ikrima.


Afisa mmoja wa Marekani ambaye hakutaka kutajwa jina lake, hajasema sehemu ambayo ndege hiyo isiyoruka na rubani ilianzia safari yake, lakini jeshi la Marekani huendesha shughuli zake za ndege hizo kutoka kambi za nchini Djibouti na Arba Minch kusini mwa Ethiopia.


Wapiganaji wa al-Shabaab wametimuliwa kutoka miji mikuu ya Somalia, ikiwa ni pamoja na Mogadishu na bandari ya kusini mwa nchi hiyo Kismayo, kufuatia operesheni ya jeshi la Umoja wa Afrika linalosimamiwa na Umoja wa Mataifa na ambalo sasa lina wanajeshi 17,700.


Kundi hilo hata hivyo linayadhibiti maeneo makubwa ya kusini mwa Somalia na katika kipindi cha miezi kadhaa iliyopita, limekiongeza kiwango cha mashambulizi yake ya kujitoa mhanga. DW

Tuesday, October 22, 2013

Blind Tunisian woman regains eyesight in Arafat



Nafeesa Al-Qurmazi

Khaled Saleem Al-Humaidi
Okaz/Saudi Gazette



HOLY SITES — After 18 months of living in complete darkness, a Tunisian woman pilgrim regained her eyesight while standing on Arafat at the climax of the Haj.
The 70-year-old Nafeesa Al-Qurmazi, mother of two boys and three girls, said she came to the Kingdom for Haj totally blind and is now going back to Tunisia with her full eyesight.

She lost her eyesight after she had a stroke about a year and a half ago. The doctors lost all hope that she would regain eyesight due to the severity of the stoke and her age.

"I have never lost hope in the providence of Allah. I kept praying to Him all the time to give me back my eyesight," she said.

Qurmazi said she decided to increase her Duaa (supplication) in Arafat and was sure that “Allah would not disappoint me. While doing the Duaa in Arafat I suddenly started to see. When the other pilgrims in my tent saw me crying with joy, they all started chanting  Allahu Akbar," she said.

Qurmazi said all the way from Tunisia she had been cherishing one dream: To see the holy sites, Makkah and Madinah. "Thank God now I can see and walk anywhere without any assistance from anyone," she said.

She said she was overjoyed to see the pilgrims in Arafat, a scene she never expected to be true to her. "Allah has blessed me with my eyesight in the most sacred place on earth," she said.

Monday, October 21, 2013

Amnesty yakosoa ukiukaji haki za binadamu Saudia


Amnesty yakosoa ukiukaji haki za binadamu  Saudia
Shirika la Msamaha Duniani (Amnesty International) limeikosoa Saudi Arabia kwa kutokomesha hali ya kutisha ya haki za binadamu nchini humo. Amnesty International imetoa ripoti iliyoiwasilisha kwa Umoja wa Mataifa ikibainisha ukandamizaji na uvunjaji wa haki za binadamu dhidi ya raia wa Saudi Arabia kama vile kutiwa mbaroni  na kushikiliwa kiholela, kukatiwa hukumu zisizo za kiadilifu na mateso mengine katika kipindi cha miaka iliyopita. Amnesty International imewasilisha ripoti yake hiyo kwa Umoja wa Mataifa kuhusu uvunjaji wa haki za binadamu nchini Saudia Arabia kabla ya kuanza mkutano wa umoja huo uliopangwa kufanyika hii leo Jumatatu huko Geneva Uswisi, kuchunguza hali ya haki za binadamu huko Saudia. Ukandamizaji mwingine uliotajwa kwenye ripoti hiyo ni kuhusu wimbi jipya la ukandamizaji dhidi ya wananchi huko Saudi Arabia katika kipindi cha miaka miwili ya hivi karibuni.

Boko Haram yaua 19 kaskazini mashariki mwa Nigeria


Boko Haram yaua 19 kaskazini mashariki mwa Nigeria
Watu wasiopungua 19 wameuawa katika mashambulizi yaliyofanywa na wanamgambo wa kundi la Boko Haram huko kaskazini mashariki mwa Nigeria. Hayo yameelezwa na wenyeji na watu walionusurika na nmashambulizi hayo. Hadi sasa miili 19 imegunduliwa katika eneo palipojiri mashambulizi hayo ya Boko Haram. Habari zinasema kuwa wanamgambo wa kundi la Boko Haram walifunga barabara kuu karibu na mji wa Logumani umbali wa kilomita 30 kutoka katika mpaka wa Nigeria na Cameroon na kuanza kuua raia na kuchoma moto malori matatu. Wahanga watano ambao miongoni mwao walikuwa ni madereva wawili wa malori na wasaidizi wao waliuliwa kwa kupigwa risasi na waliosalia walichinjwa. Boko Haram imetekeleza mashambulizi hayo jana katika hali ambayo tarehe sita mwezi huu pia kundi hilo liliushambulia msikiti mmoja huko Damboa katika jimbo la Borno na kuwauwa waumini watano waliokuwa katika sala ya asubuhi. 

41 wauliwa katika mashambulizi Sudan Kusini


41 wauliwa katika mashambulizi Sudan Kusini Watu wasiopungua 41 wameuawa na wengine 63 kujeruhiwa katika mashambulizi ya silaha yaliyotekelezwa katika jimbo la Jonglei mashariki mwa Sudan Kusini. Ripoti za awali zinaeleza kuwa watu 41 wameuawa na wengine 63 kujeruhiwa, huku hali ya baadhi ya majeruhi zikiwa mbaya sana. Hussein Maar Kaimu gavana wa jimbo la Jonglei amesema kuwa kuna uwezekano wa baadhi ya majeruhi ambao hali zao ni mbaya sana wakaaga dunia wakati wowote. Maar ameongeza kuwa wavamizi walikuwa na silaha za otomatiki na kwamba waliiba maelfu ya ng'ombe kwenye shambulizi hilo. Kaimu gavana wa jimbo la Jonglei ambalo ni jimbo kubwa zaidi huko Sudan Kusini amesema kuwa wanamgambo wanaoongozwa na David Yau Yau wanashukiwa kuhusika na shambulio hilo. 

TAZAMA PICHA 7 ZA WALE WATANZANIA 11 WALIOKAMATWA WAKIFANYA MAZOEZI YA KIJESHI KWA KUTUMIA CD ZA AL SHABAAB NA ALQAEDA ....



Hawa  ni  vijana  wa  kitanzania 11  ambao  walikamatwa  na  jeshi la polisi   Mtwara baada ya  kupata taarifa kwamba  walikua wakifanya mazoezi ya kivita kwa kutumia CD za  Al Qaeda na Al Shabaab ambapo walikamatwa na hizo CD  pamoja  na  silaha   mbalimbali  kama  ushahidi...

Taarifa ya jeshi la Polisi leo  imesema kuwa , vijana  hawa walipelekwa Mahakamani na watarudishwa tena tarehe 4 November 2013.

 
 
 
 
 
 

TAARIFA ZA MSIBA

Leo ametutoka Mwanachuoni  Mkubwa katika Wanachuoni wa Madh-hab ya Imamu Shafiih , Mwanachuoni ambaye Ni rejeo katika Elimu ya Fiqh na Usuul l fiqh Sheikh Ahmad bin Abdullahi Adughaan M/Mungu Amrehemu na Ampokee  Mapokezi Mema na Ampe Pepo ya Daraja ya Juu yeye pamoja na Wazazi wetu wote waliotangulia Mbele ya Haki awakutanishe na  Mtume Muhammad (S.A.W) Rehma za M/Mungu zimshukie Juu yake na Amani pamoja na Waja Wema.
Amiin .
Amefia katika Nchi ya Saudia Arabia.

انتقل اليوم إلى رحمة الله مُفتي السّادة الشّافعية بالأحساء الإمام العارف بالله الفقيه الأصولي المُسند المُحقّق الجليل، أستاذ الأجيـــال ومُجدّد المدرسة الشافعية بشرق المملكة العربية السعودية،الشيخ أحمد بن عبد الله الدُّ وغـــان الخالدي الأحسائي الأشعري الشافعي

رحمه الله تعالى وأسكنه الفردوس الأعلى وجزاه عنا وعن طلابه خير الجزاء.

Saturday, October 19, 2013

Rais Uhuru Kenyatta kutohudhuria vikao ICC


Rais Uhuru Kenyatta kutohudhuria vikao ICCMahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC imechukua uamuzi wa kumsamehe Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya asihudhurie vikao vya kesi inayomkabili huko Hague nchini Uholanzi. Taarifa iliyotolewa jana na mahakama hiyo imeeleza kuwa, Rais Kenyatta atahudhuria kikao cha ufunguzi wa kusikiliza kesi yake na kikao cha mwisho cha kutolewa hukumu ya kesi inayomkabili. Awali, Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC ilimtaka Rais Kenyatta ahudhurie mwenyewe kwenye kwenye vikao vyote ya kesi inayomkabili, ambayo imepangwa kuanza kusikilizwa tarehe 12 Novemba mwaka huu. Hivi karibuni, Umoja wa Afrika uliitaka Mahakama ya Kimataifa ya Jinai kusitisha zoezi la kusikiliza kesi za Rais Kenyatta na Naibu wake William Ruto, hadi pale viongozi hao watakapoondoka madarakani. Viongozi hao wa Kenya wanatuhumiwa kwa kufanya uchochezi na kusababisha mauaji ya watu wasiopungua 1,500 katika machafuko yaliyojiri Kenya mara baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2007.

Waziri wa Sheria wa Ufaransa afananishwa na nyani


Waziri wa Sheria wa Ufaransa afananishwa na nyaniMgombea wa chama chenye misimamo mikali cha Nation Front nchini Ufaransa amepigwa marufuku kushiriki kwenye kinyang'anyiro cha uchaguzi wa mabaraza ya miji, uliopangwa kufanyika mwezi Machi mwaka 2014, baada ya kumvunjia heshima Waziri wa Sheria wa nchi hiyo kwa kumfananisha na nyani.
Anne Sophie Leclere mgombea wa nafasi ya udiwani katika eneo la Rethel kwa tiketi ya chama cha Nation Front amezuiwa kushiriki kwenye kinyang'anyiro hicho baada ya kutoa taswira ya mtoto wa nyani kwenye ukurasa wake wa Facebook, akiwa na lengo la kumfananisha na Bi. Christiane Taubira Waziri wa Sheria wa Ufaransa mwenye asili ya Guinea. Chama cha National Front cha Ufaransa kinachoongozwa na Marine Le Pen hivi karibuni kimepata umashuhuri na uungaji mkono mkubwa wa wananchi wa Ufaransa kutokana na sera zake za kuwa dhidi ya wahajiri na kupinga siasa za Umoja wa Ulaya.
Inafaa kukumbusha kuwa, Cecile Kyenge Waziri wa Mshikamano wa Italia ambaye ni waziri wa kwanza mweusi, miezi michache iliyopita pia alikumbana na vitendo vya kibaguzi, baada ya Roberto Calderoli Naibu Spika wa Baraza la Seneti la Italia kumfananisha na nyani mwanamama huyo mwenye asili ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

Saudi Arabia kumkata kichwa hujaji wa Iraq


Saudi Arabia kumkata kichwa hujaji wa IraqHatua ya Saudi Arabia ya kutoa hukumu ya kukatwa kichwa hujaji wa Iraq, baada ya kukamatwa na askari wa Saudia kwenye makaburi ya Baqii, imekabiliwa na radiamali kali ya bunge la Iraq. Kamisheni ya Uhusiano wa Kigeni ya Bunge la Iraq imeeleza kuwa, hukumu hiyo iliyotolewa dhidi ya hujaji huyo wa Iraq inaonyesha jinsi utawala wa Saudia ulivyokuwa na chuki dhidi ya Waislamu wa Madhehebu ya Shia. Sami al Askari mjumbe wa kamisheni hiyo amesema kuwa, utawala wa Saudi Arabia hauna haki ya kutoa hukumu kama hiyo ya kukatwa kichwa hujaji huyo wa Iraq. Al Askari ameongeza kuwa, watawala wa Saudia wana chuki na uadui dhidi ya Mashia kutoka Lebanon, Iran, Iraq na hata wale walioko ndani ya nchi hiyo.
Ameongeza kuwa, nchi za Magharibi ambazo zimekuwa zikijinadi kutetea haki za binadamu zimekuwa zikifumbia macho  jinai na ukiukwaji wa haki za binadamu nchini humo, kwa vile watawala wa nchi hiyo ni vibaraka wa Magharibi.
Inafaa kuashiria hapa kuwa, Salam Kadhim hujaji kutoka Iraq alikamatwa na askari wa Saudi Arabia akiwa analia kwenye makaburi ya Baqii, ambapo mahala hapo wamezikwa watu wa Nyumba Tukufu ya Mtume Mtukufu SAW. Hukumu hiyo ya kukatwa kichwa, ilipangwa kutekelezwa mara tu baada ya kumalizika ibada ya hija.

Wednesday, October 16, 2013

MUME AMKATA MKEWE MGUU HUKO TARIME MKOANI MARA



 Ghati Chacha (21) mkazi wa kijiji cha Nyanitira kata ya Nyansincha Wilayani Tarime amesababishiwa kilema cha maisha kwa kukatwa mguu wake wa kulia na Mume wake baada ya kuchelewa kumfungua mlangao nyakati za usiku.

Akisimulua mkasa huo hivi karibuni akiwa wodi namba sita alikolazwa akiuuguza vidonda na majeraha,Ghati alisema, mume wake  aliye mtaja kwa majina ya Chacha Mwita(23) alifika nyumbani saa mbili usiku akiwa amelewa.

Rais Kikwete ashiriki Swala ya EID el Adh- ha jijini Dar leo katika Msikiti wa Maamour Upanga .

 Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na baadhi ya waumini wa dini ya Kiislamu muda mfupi baada ya kushiriki Swala ya EID iliyofanyika katika msikiti wa Maamour Upanga jijini Dar es Salaam leo asubuhi .
Picha na  Freddy Maro.
chanzo:- http://kkiislamtnz.blogspot.com

Kisima cha ajabu mkoani Dodoma


KISIMANI 1 f3a53
Koo mbili za Wanyazaga na Wambukwa mnyambwa wakiwa wamekusanyika kukizunguka kisima kinachosemekana kimejaa maajabu cha Bwibwi kilichopo Katika kijiji cha Iyumbu kilichopo pembezoni mwa Chuo kikuu cha Dodoma
[UDOM] 
MAJI 1 fb354
Baadhi ya wananchi wakifurahia kutumia maji yanayopatikana kisima cha Bwibwi kilichopo katika kijiji cha iyumbu Manispaa ya Dodoma, kisima hicho kilichovumbuliwa katikati ya miaka 1,800 kiko katika hatihati ya kufukiwa na eneo hilo lituumike kwa matumizi mengine.
MAJI 2 f8953
Mkuu wa kimila wa kabila la kigogo Lazaro Chihoma akinywa maji yaliyochotwa kisima cha Bwibwi kilichopo Kijiji cha Iyubu Manispaa ya Dodoma, Kisima hicho kinachoaminika ni cha maajabu na mtu anayetumia maji yake hupata Mafanikio ya kiafya na kimaisha: PICHA NA JOHN BANDA

Monday, October 14, 2013

Haramain Salaat Recordings: Kiswa Change - 1434

Haramain Salaat Recordings: Kiswa Change - 1434: Yawm al 'Arafah 1434 Audio background: Makkah Isha Salah by Sheikh Baleela from 8th Dul Hijjah 1434

Walowezi wa Israel wavamia Msikiti wa al Aqswa


Walowezi wa Israel wavamia Msikiti wa al Aqswa
Makumi ya walowezi wa Kizayuni wenye misimamo ya kufurutu ada wamevamia Msikiti Mtukufu wa al Aqswa huko mashariki mwa Quds na kupeperusha bendera za Israel ndani ya msikiti huo.
Ripoti zinasema kuwa, tukio hilo limejiri leo na baada ya hapo polisi ya Israel ilifunga mlango wa Magharba unaotumiwa na wageni kuingia ndani ya msikiti huo mtukufu.
Tukio kama hilo pia lilishuhudiwa Septemba 18, ambapo askari wa utawala ghasibu wa Israel waliva uwanja wa msikiti huo na kuwapulizia gesi za kutoa machozi waumuni wa Kipalestina.
Msikiti wa al Aqswa uliopo katike mji wa al Quds unaokaliwa kwa mabavu na Israel umekuwa kitovu cha vurugu na machafuko. Mayahudi wanataka kubomoa msikiti huo ambao ni kibla cha kwanza cha Waislamu kwa kisingizio cha kutafuta mabaki ya hekalu la Nabii Sulaiman.  

Swala na Sherehe za Eid Leicester, England



Assalaamu Alaykum,

Wapenzi Waislamu wa mji wa Leicester na vitongoji vyake, kwa mara nyingine

 JUMUIA YA ANNOOR LEICESTER ina furaha kukualikeni katika

Sherehe za Eid ul Adh-ha hapo JUMANNE 15 Oktoba 2013

Ambazo kwa mara ya kwanza katika historia zitafanyika katika jengo letu jipya Inshaallah.

EID TAKBEER zitaanza saa mbili na robo asubuhi (8.15am)

SALA YA EID itasaliwa saa tatu kasorobo asubuhi (8.45am)

STAFTAHI ya pamoja baada ya Sala

ANWANI: Masjid An Noor Leicester, 170a Belgrave Gate, Leicester, LE1 3XL

Tafadhali wasiliana nasi kwa mchango wako kama kawaida ya miaka yote

Asaa Kakuzi 07951 644936

Malik 07983 614261


EID MUBAARAK !! KULLU AM WA ANTUM BIKHAYR !!

Nahodha ashangazwa ufisadi kufumbiwa macho ZNZ


Nahodha ashangazwa ufisadi kufumbiwa macho ZNZ
Shamsi Vuai Nahodha Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameelezea kushangazwa kwake na hatua za kutochukuliwa watu waliohusika na ufisadi wa Sh60 bilioni wakati wa utawala wa Rais Amani Abeid Karume. Akihutumia mkutano wa hadhara mjini Unguja, Nahodha amesema ufisadi huo ulibainika baada ya uchunguzi wa Kamati Teule ya Baraza la Wawakilishi.
Nahodha amesema ripoti hiyo ilitaja hadi waliohusika na ufisadi huo lakini hakuna hatua  zozote zilizochukuliwa hadi leo. Nahodha ametoa tuhuma hizo licha ya ukweli kuwa kipindi cha utawala wa Rais Karume, alikuwa Waziri Kiongozi kwa miaka 10. Waziri huyo wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa wa Tanzania amesema kuwa, dhana ya kufanyika Mapinduzi ya Zanzibar mwaka 1964 ilikuwa ni kuimarisha huduma za jamii kama utoaji wa elimu bure, umiliki wa ardhi kwa wananchi wanyonge na kupinga vitendo vya ubaguzi na matabaka.

Sudan kuimarisha usalama eneo la Darfur Mashariki


Sudan kuimarisha usalama eneo la Darfur Mashariki
Jeshi la Sudan limepeleka askari zaidi huko Mashariki mwa eneo la Darfur kwa lengo la kuimarisha usalama zaidi wa raia wakati huu wa sikukuu ya Idil Adha. 
Bilal Saed Daqis ambaye ni miongoni mwa maafisa wa Darfur amesema kuwa, wanajeshi zaidi wamepelekwa mashariki mwa eneo hilo ili kuzuia machafuko kati ya makabila ya al Manaliya na ar Razqat na kuimarisha usalama zaidi.
Wakati hayo yanaripotiwa askari watatu wa kikosi cha kulinda amani wa Umoja wa Mataifa UNAMID wanaotoka Senegal wameuawa katika shambulio lililofanywa dhidi ya msafara wa umoja huko kwenye eneo la Darfur. Mwakilishi maalumu wa kikosi cha UNAMID Mohamed Ibn Chambas amesema kwamba, shambulizi hilo ni jinai na kwamba serikali ya Sudan inapaswa kuchukua hatua muhimu ili kuzuia mashambulizi kama hayo.

Wawili wauawa kwenye mlipuko Addis Ababa


Wawili wauawa kwenye mlipuko Addis AbabaWatu wawili wameuawa katika mlipuko wa bomu uliotokea mjini Addis Ababa, Ethiopia.
Jeshi la polisi la Ethiopia limetangaza kuwa, uchunguzi umeshaanza ili kubaini sababu za kutegwa bomu hilo ambalo limelipuka katika eneo la Bole. Hadi sasa hakuna kundi lolote lililotangaza kuhusika na mlipuko huo. Hata hivyo, viongozi wa serikali wanalituhumu kundi la waasi lililoko kusini na kusini mashariki mwa nchi hiyo kwa kuhusika na ulipuaji mabomu nchini Ethiopia.
Inafaa kuashiria hapa kuwa, mwezi Novemba 2011 Ethiopia ilipeleka vikosi vya dhiba nchini Somalia kwa shabaha ya kulisaidia jeshi la nchi hiyo, kwenye mapambano dhidi ya kundi la al Shabab. Hivi karibuni Hailemariam Deslaegn,Waziri Mkuu wa Ethiopia amesikika akisema kuwa, Addis Ababa haitayaondoa majeshi yake nchini Somalia, hadi pale amani itakaporejea nchini humo.

Saturday, October 12, 2013

Njama ya kujenga hekalu Quds tukufu yalaaniwa


Njama ya kujenga hekalu Quds tukufu yalaaniwaTaasisi mbalimbali za Palestina zimelaani njama ya utawala wa Kizayuni wa Israel ya kutaka kujenga hekalu katika eneo la mashariki ya msikiti mtukufu wa al Aqsa. Baraza Kuu la Kiislamu, Baraza la Waqfu na Masuala ya Kiislamu na Baraza la Fatwa la Quds tukufu yametoa taarifa ya pamoja leo ambapo mbali na kufichua, yamelaani pia njama hiyo ya utawala wa Kizayuni dhidi ya kibla cha kwanza cha Waislamu. Taarifa hiyo imeashiria kubadilishwa sura ya sehemu ya msikiti huo ya al Buraq na vilevile kujengwa njia ya mabasi yaendayo kwa kasi katika eneo la kati ya Jabalu-turi na Babul-asbat, na kueleza kuwa miradi hiyo inatekelezwa kwa lengo la kuyayahudisha maeneo matakatifu na kufuta athari za Kiislamu, kitu ambacho hakikubaliki. Taarifa ya taasisi hizo za Palestina imeashiria mpango wa Israel wa kujenga hekalu katika eneo la sehemu moja ya tano ya msikiti wa Alqsa na kusisitiza kwamba msikiti huo kidini, kisiasa na kimamlaka hauna uhusiano wowote na Mayahudi na kwamba eneo hilo takatifu la Baitul Muqaddas ni milki ya Waislamu wote duniani. Sambamba na kutoa indhari kwa utawala wa Kizayuni juu ya mas-ulia utakayobeba kwa hatua yoyote ya kuuvunjia heshima msikiti mtukufu wa al Aqsa, taarifa hiyo imetoa wito pia kwa Ulimwengu wa Kiislamu na wa Kiarabu kutimiza wajibu walionao juu ya msikiti huo mtakatifu pamoja na Quds tukufu…/

'Watanzania ni miongoni mwa watu wasio na furaha'


'Watanzania ni miongoni mwa watu wasio na furaha'
Ripoti iliyotolewa na Umoja wa Mataifa inaonesha kuwa, Watanzania ni miongoni mwa watu wasio na furaha na waliokata tamaa hapa duniani. Ripoti hiyo imeitaja Tanzania kuwa ni miongoni mwa nchi 10 za mwisho duniani kati ya nchi 156 zilizofanyiwa utafiti huo. Upatikanaji wa huduma za jamii, mtazamo wa watu kuhusu rushwa, umri wa kuishi, ukosefu wa kazi, pato la taifa na ukarimu wa watu katika nchi husika, ni baadhi ya vigezo vilivyoangaliwa wakati wa kuandaa ripoti hiyo. Taarifa hiyo imezitaja nchi tano za Denmark, Norway, Uswisi, Uholanzi na Sweden kuwa ndizo zinazoongoza kwa watu wake kuwa na furaha zaidi duniani, huku Angola ikishika nafasi ya kwanza Afrika na ya 61 duniani. Kwa upande wa Afrika Mashariki, wananchi wa Uganda ndio walionekana kuwa na furaha zaidi katika ripoti hiyo kwani nchi hiyo imeshika nafasi ya 120 wakifuatiwa na Kenya iliyoshika nafasi ya 123, Tanzania nafasi ya 151, Rwanda nafasi ya 152 na Burundi ni ya mwisho Afrika Mashariki huku ikiwa inashikilia nafasi ya 153 duniani. Hata hivyo, Waziri wa Kazi na Ajira wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Gaudensia Kabaka ameeleza kushtushwa na ripoti hiyo akisema kuwa ni asilimia 11.7 tu ya Watanzania wasio na ajira na kwamba, wale wanaofanya kazi, wanapata huduma zote za msingi, ikiwa ni pamoja na kwenda likizo na mishahara inayolingana na taaluma zao na kusisitiza kwamba, hafahamu ni vigezo vipi vimetumika katika ripoti hiyo.

AU: ICC isiwashtaki viongozi walioko madarakani


AU: ICC isiwashtaki viongozi walioko madarakaniViongozi wa nchi wanachama wa Umoja wa Afrika AU wanaokutana makao makuu ya umoja huo mjini Addis Ababa, Ethiopia wameitaka Mahakama ya Kimataifa ya Jinai ICC isiwafungulie mashtaka viongozi wa nchi za Afrika wanapokuweko madarakani. Viongozi hao aidha wameitaka mahakama hiyo iakhirishe kesi za marais wa Uhuru Kenyatta wa Kenya na Omar al Bashir Sudan. Mkuu wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika Bi Dlamini Zuma, amesema Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na Mahakama ya Kimataifa ya Jinai zinapaswa kuakhirisha haraka usikilizaji wa kesi za viongozi wa Kenya waliochaguliwa na wananchi. "Baraza la Usalama na ICc zinapaswa kushirkiana nasi ili kuwezesha uongozi wa Kenya uliochaguliwa na wananchi uweze kutekeleza majukumu yake ya kikatiba kwa kulizingatia kwa haraka suala la uakhirishaji kesi zinazosikilizwa na ICC dhidi ya Rais na Makamu wa Rais wa Kenya", amesema Zuma. Mbali na Rais, Naibu wa Rais wa Kenya William Ruto naye pia anakabiliwa na kesi katika Mahakama ya Kimataifa ya Jinai yenye makao yake the Hague, Uholanzi ya kuhusika na kuongoza machafuko ya baada ya uchaguzi mkuu wa Kenya wa mwaka 2007 yaliyosababisha vifo vya zaidi ya watu 1,200…/

Dola milioni 500, pato la M23 kwa magendo ya madini


Dola milioni 500, pato la M23 kwa magendo ya madini
Gazeti la Los Angeles Times linalochapishwa nchini Marekani limeandika kuwa waasi wa M23 walioko mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo hujipatia takribani dola milioni 500 kila mwaka kutokana na magendo ya dhahabu nchini humo. Uchunguzi uliofanywa na taasisi ya  kutetea haki za binadamu ya Enough ya Washington nchini Marekani unaonyesha kuwa, waasi wa M23 waliojizatiti mashariki mwa nchi hiyo hufanya magendo ya madini ya dhahabu na kujipatia mamilioni ya dola kila mwaka, pesa ambazo hutumiwa kununulia silaha na kufanya jinai na mauaji ya halaiki katika  eneo hilo. Taasisi hiyo imeeleza kuwa, licha ya kinara wa kundi hilo Bosco Ntaganda kupelekwa kwenye mahakama ya ICC kwa tuhuma za kutenda jinai za kivita, lakini wasaidizi wake wamefanikiwa kutorosha kwa njia za magendo dhahabu za Kongo na kuziuza nchini Imarati, kupitia nchi jirani za Burundi na Uganda. Uchunguzi huo umeeleza kuwa, kila mwaka tani 12 za magendo ya madini ya dhahabu yenye thamani ya dola milioni 500 hupelekwa nje ya nchi hiyo kinyume cha sheria. 

AU kuongeza askari wa AMISOM nchini Somalia


AU kuongeza askari wa AMISOM nchini SomaliaUmoja wa Afrika unapanga mikakati ya kuongeza idadi ya askari wa kulinda amani nchini Somalia AMISOM, kwa shabaha ya kupambana na wanamgambo wa kundi la al Shabab nchini humo. Tokea mwaka 2007, kikosi cha AMISOM  kiko nchini Somalia, na katika miaka miwili ya hivi karibuni kimefanya operesheni kadhaa  dhidi ya wanamgambo wa kundi hilo. Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika limetangaza kuwa wataongezwa askari 6,235 na kuifanya idadi ya wanajeshi walioko nchini humo kufikia elfu ishirini na tatu mia tisa na sitini na sita.
Hata hivyo uamuzi huo unapaswa kuthibitishwa na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa. Imeelezwa kuwa gharama za kuendesha operesheni za AMISON zinadhaminiwa na Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika na wanajeshi wengi wa kikosi hicho wanatoka nchi za Uganda, Burundi na Kenya. Kundi la al Shabab limeshadidisha operesheni zake dhidi ya majeshi ya kigeni na hasa baada ya kupoteza udhibiti wa ngome zake hasa hasa katika maeneo ya kusini mwa nchi hiyo.

Wednesday, October 9, 2013

Ikhwan yaondolewa katika orodha ya NGO Misri


Ikhwan yaondolewa katika orodha ya NGO Misri
Harakati ya Ikhwanul Muslimin sasa imefutwa kikamilifu nchini Misri baada ya serikali kuamuru kundi hilo liondolewe katika orodha ya mashirika yasiyo ya kiserikali NGO nchini humo.  Uamuzi huo wa serikali ya Misri wa kuiondoa Ikhwanul Muslimin katika orodha ya NGO umechukuliwa siku kadhaa baada ya kundi hilo la kisiasa kupigwa marufuku.
Baada ya kuingia madarakani serikali ya mpito inayoungwa mkono na jeshi nchini Misri zimechukuliwa hatua kali dhidi ya harakati ya Ikhwan hasa baada ya kupinduliwa rais wa zamani wa nchi hiyo aliyechaguliwa na wananchi Muhammad Musri mwezi Julai. Wengi wanaamini kuwa uamuzi huo sasa unaandaa mazingira ya jeshi la Misri kuwatia mbarozi zaidi wafuasi wa harakati ya Ikhwanul Muslimin.

Mhadhiri Saudia ahukumiwa kwa kumnajisi binti yake


Mhadhiri Saudia ahukumiwa kwa kumnajisi binti yake
Mhadhiri mmoja wa kidini nchini Saudi Arabia amehukumiwa kifungo cha miaka minane jela na kuchapwa viboko 800 kwa kosa la kumnajisi bintiye mdogo wa miaka mitano na kumtesa hadi kufariki dunia. Mahakama ya Saudi Arabia Jumatatu hii ilimuamuru Fayhan al Ghamdi kumlipa mke wake wa zamani yaani mama wa binti huyo fedha za diya ya damu dola za Kimarekani 270,000. Mke wa pili wa mahdhiri huyo aliyekutwa na hatia ambaye naye ameshtakiwa kwa kushiriki kwenye jinai hiyo amehukumiwa kifungo cha miezi kumi jela na viboko 150. Binti huyo wa Saudia aliyekuwa na umri wa miaka mitano alilazwa hospitali mwezi Disemba mwaka juzi akiwa na majeraha kadhaa, michubuko, majeraha ya kuungua moto na kupasuka fuvu la kichwa. Wanaharakati nchini Saudi Arabia na wa nchi za nje wamelaani vikali jinai hiyo iliyofanywa na baba huyo kwa bintiye na kuitaja adhabu iliyotolewa na mahakama ya nchi hiyo kwa mtenda jinai huyo kuwa ya kiwango cha chini mno. Wanaharakati hao wamesema mtenda jinai huyo alipaswa kufungwa jela maisha au kunyongwa ili iwe mfano kwa wengine.

Waliokufa kwenye ghasia Sudan ni 70


Waliokufa kwenye ghasia Sudan ni 70Afisa wa serikali ya Sudan ametangaza kuwa, idadi ya watu waliouawa katika machafuko ya hivi karibuni mjini Khartoum yaliyoanza wakati wa maandamano Septemba 23 ni 70. Abdurahman al Khadr Gavana wa jiji la Khartoum ameongeza kuwa idadi hiyo imethibitishwa na Wizara ya Afya ya nchi hiyo na kwamba uchunguzi zaidi unafanywa ili kufahamu sababu kuu zilizosababisha machafuko hayo.
Maandamano yalianza nchini Sudan baada ya bei ya mafuta ya petroli kupanda karibu mara dufu. Nchi hiyo ilipoteza mabilioni ya dola baada ya Sudan Kusini kujitenda mwaka 2011, na inasemekana kuwa tangu wakati huo serikali ya Khartoum imekuwa ikikabiliwa na mfumoko wa bei, kuanguka thamani ya sarafu na kupungua akiba ya pato la kigeni.
HII NDIO TAARIFA YA POLISI KUHUSU VIJANA WALIOKAMATWA WAKIFANYA ZOEZI POLINI HUKO MTWARA Written By umar makoo on Wednesday, October 9, 2013 | 4:42 AM 45 3 1 Hizi ni moja ya CD zilizokamatwa na askari wa jeshi la polisi Mtwara ikiwemo na kuwakamata vijana 11 ambao wanadaiwa walikua wakifanya mazoezi ya kijeshi waliyokua wakijifunza kutoka kwenye CD za magaidi zilizokua na mafunzo kutoka kwa makundi ya Al Shabaab na Al Qaeda. Taarifa zaidi unaweza kuzisoma hapo chini kwenye hiyo taarifa iliyotolewa na jeshi la polisi. 2

Original from: http://www.googlehabari.blogspot.com/2013/10/hii-ndio-taarifa-ya-polisi-kuhusu.html
Copyright EXEIdeas - All Ri

Tuesday, October 8, 2013

Rwanda yatakiwa iache kuwasaidia waasi Kongo DRC


Rwanda yatakiwa iache kuwasaidia waasi  Kongo DRC
Marekani imeitaka serikali ya Rwanda kutoa ushirikiano utakaosaidia kukomeshwa mapigano huko Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Samantha Power, mwakilishi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa amesema kuwa, Rwanda ikiwa ni nchi jirani na Kongo inapaswa kuwa na nafasi ya moja kwa moja katika mchakato wa kuleta amani na utulivu nchini Kongo. Bi. Power amesisitiza kwamba nchi zote za eneo la Maziwa Makuu ya Afrika zinapaswa kufanya juhudi maradufu za kuwatokomeza waasi walioko mashariki mwa nchi hiyo. Hapo jana ujumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa uliyataka makundi ya waasi mashariki mwa Kongo kuacha kuendeleza machafuko katika eneo hilo. Inafaa kuashiria hapa kuwa, mazungumzo ya amani kati ya serikali ya Kongo na waasi wa M23 kwa upatanishi wa Uganda bado yanaendelea, lakini hadi sasa hayajakuwa na natija yoyote ile. 

Makanisa ya Kenya yajitosa kwenye mgogoro wa ICC


Makanisa ya Kenya yajitosa kwenye mgogoro wa ICCViongozi wa makanisa nchini Kenya wamemtaka Rais Uhuru Kenyatta kutoshirikiana na Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) yenye makao yake mjini Hague, Uholanzi.
Wakiongozwa na Askofu Mkuu wa kanisa la AIPCK,  Mugecha Karume, viongozi hao wa makanisa  wamesema kuwa, kesi hiyo ina  mambo mengi yasiyoeleweka na kwa mantiki hiyo, hakuna haja Rais Kenyatta kwenda Hague kwa ajili ya kesi dhidi yake mbele ya mahakama hiyo.
Rais Uhuru Kenyatta, Naibu wake William Ruto na mtangazaji wa radio Joshua Sang wanakabiliwa na mashtaka ya kuhusika na ghasia za baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2007 ambapo zaidi ya Wakenya 1000 waliuawa. Kwa sasa Naibu Rais wa Kenya, William Ruto na Joshua Sang wako mjini Hague ambako kesi zao zinaendelea. Kesi ya Rais Kenyatta inatarajiwa kunza mwezi ujao wa Novemba. Umoja wa Afrika AU pia umetaka kesi hizo zisimamishwe au kuhamishiwa jijini Nairobi ili zisikizwe na mahakama za Kenya.

UN na AU kujadili mgogoro wa Sudan Mbili


UN na AU kujadili mgogoro wa Sudan Mbili
Wawakilishi kutoka Umoja wa Afrika  na  wale wa Umoja wa Mataifa watakutana leo Addis Ababa mji mkuu wa Ethiopia kwenye kikao cha kila mwaka, ambapo mwaka huu ajenda kuu itakuwa ni kuujadili kwa kina mgogoro wa  mpaka kati ya nchi za Sudan na Sudan Kusini. Taarifa iliyotolewa na Umoja wa Afrika imeeleza kuwa, licha ya mgogoro wa Sudan mbili,  wajumbe wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika watajadili pia hali ya mambo katika eneo la Maziwa Makuu ya Afrika, Pembe ya Afrika, Jamhuri ya Afrika ya Kati na eneo la Sahel. Sudan Kusini ambayo awali ilikuwa sehemu ya Sudan, ilijitangazia uhuru wake mwezi Juni 2011. Hata hivyo, nchi hizo mbili zimetumbukia kwenye mgogoro mkubwa baada ya kila upande kudai haki ya umiliki wa maeneo matano ya mpakani na hali kadhalika tuhuma za kila upande za kuwaunga mkono waasi wa upande wa pili. Hadi sasa, Sudan imeshaishitaki Sudan Kusini mara tano kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa kuwaunga mkono wapinzani wa serikali ya Khartoum.

Kenya kutoa zawadi kwa wafichuaji wa Westgate


Kenya kutoa zawadi kwa wafichuaji wa Westgate
Polisi ya Kenya imetangaza kuwa iko tayari kutoa kitita cha shilingi laki tano za nchi hiyo ambazo ni sawa na dola 5, 827 kwa mtu atakayetoa taarifa zitakazosaidia kukamatwa mwenye gari linalosadikiwa kutegwa  mabomu kwenye shambulio lililofanywa zaidi ya wiki mbili zilizopita kwenye jumba la biashara la Westgate jijini Nairobi, Kenya.  Mkuu wa kikosi  maalumu cha kupambana na ugaidi nchini Kenya ameeleza kuwa, gari hilo linashukiwa  lilikuwa limesheheni mada za milipuko na silaha na kuongeza kuwa kikosi hicho bado kinaendelea kumsaka mmiliki wa gari hilo.  Amesema kuwa, awali mmiliki wa gari hilo alikuwa Mkenya mwenye asili ya Kisomali. Kundi la al Shabab la nchini Somalia lilitangaza kuhusika na shambulio hilo lililopelekea watu wasiopungua 67 kuuawa ingawa hadi sasa watu wengine 39 waliokuwepo kwenye eneo hilo hawajulikani walipo. Kundi la al Shabab limeitaka serikali ya Kenya kuondoa majeshi yake nchini Somalia, kinyume cha hivyo itakabiliwa na mashambulio mengine kwenye maeneo nyeti ya nchi hiyo. Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya amesikika akisema kuwa, serikali ya Nairobi haitayaondoa majeshi yake nchini Somalia hadi pale  hali ya amani na utulivu itakaporejea nchini humo.

Watoto 362 wafariki kutokana na lishe duni Niger


Watoto 362 wafariki kutokana na lishe duni Niger
Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa, watoto 362 walio chini ya umri wa miaka mitano wamefariki dunia kutokana na lishe duni nchini Niger. Taarifa ya Umoja wa Mataifa imeeleza kuwa, watoto hao wamefariki dunia katika eneo la Zinder mashariki mwa Niger kati ya mwezi Januari hadi Septemba mwaka huu. Taarifa hiyo imeeleza kuwa, asilimia 90 ya vifo katika maeneo ya Zinder, Magaria na Mirriah inatokana na lishe duni kwa watoto walio chini ya umri wa miaka mitano. Zinder ni mji wa pili kwa wingi wa watu nchini Niger, na eneo hilo hukabiliwa mara kwa mara na ukosefu wa chakula unaosababishwa na ukame, huku watoto na wanawake wakiwa wahanga wakubwa wa balaa hilo.

Monday, October 7, 2013

MAKAMU WA RAIS MH:BILAL AFUNGUA MRADI WA UKARABATI WA NJIA ZA KUSAFIRISHA UMEME


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akikata utepe ikiwa ni ishara ya kuzindua rasmi Miradi ya ukarabati wa Vituo vya Kupoza Umeme na Ujenzi wa Njia ya kusafirisha Umeme katika Mkoa wa Kilimanjaro. Hafla hiyo ya uzinduzi imefanyika leo, Oktoba 7, 2013 katika Kituo cha kupoza umeme cha Makuyuni Wilaya ya Moshi Vijijini Tarafa ya Himo Mkoa wa Kilimanjaro. Kutoka kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Tanesco, Felician Mramba, Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo (kushoto kwa Makamu) ni Balozi wa Japan nchini, Masaki Okada na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas Gama.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na baadhi ya viongozi wakitembelea kukagua mitambi ya kusambaza umeme ya Kiyungi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifunua kitambaa ikiwa ni ishara ya kuweka Jiwe la msingi, katika uzinduzi rasmi Miradi ya ukarabati wa Vituo vya Kupoza Umeme na Ujenzi wa Njia ya kusafirisha Umeme katika Mkoa wa Kilimanjaro. Hafla hiyo ya uzinduzi imefanyika leo, Oktoba 7, 2013 katika Kituo cha kupoza umeme cha Makuyuni Wilaya ya Moshi Vijijini Tarafa ya Himo Mkoa wa Kilimanjaro. Kulia ni Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo na nyuma yao ni Balozi wa Japan nchini, Masaki Okada.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiangalia moja ya mtambo wa kisasa wa kusambaza umeme uliopo katika kituo cha Makuyuni Wilaya ya Moshi Vijijini Tarafa ya Himo Mkoa wa Kilimanjaro, wakati alipofika kituoni hapo kuzindua rasmi Miradi ya ukarabati wa Vituo vya Kupoza Umeme na Ujenzi wa Njia ya kusafirisha Umeme katika Mkoa wa Kilimanjaro, leo.
kwa picha zaidi bofya soma zaidi
akamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Kaimu Mkurugenzi wa Tanesco, Felician Mramba, wakati alipotembelea kukagua Kituo cha kusambaza Umeme cha Kiyungi, mkoani Kilimanjaro.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na baadhi ya wananchi wa Wilaya ya Moshi Vijijini, mara baada ya kuwasili kwenye Kituo cha kusambaza umeme cha Makuyuni Wilaya ya Moshi Vijijini Tarafa ya Himo Mkoa wa Kilimanjaro leo kwa ajili ya kuzindua rasmi miradi ya ukarabati wa Vituo vya Kupoza Umeme na Ujenzi wa Njia ya kusafirisha Umeme katika Mkoa wa Kilimanjaro.
Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Leonidas gama, akizungumza kabla ya kumkaribisha Waziri wa Nishati na Madidi, Prof. Muhongo, aliyemkaribisha Makamu wa Rais, kuzingumza.
Sehemu ya wananchi waliojitokeza kushuhudia uzinduzi huo.


Picha ya pamoja baada ya uzinduzi huo.
Picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Tanesco baada ya uzinduzi huo. Picha na OMR