Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Saturday, October 19, 2013

Waziri wa Sheria wa Ufaransa afananishwa na nyani


Waziri wa Sheria wa Ufaransa afananishwa na nyaniMgombea wa chama chenye misimamo mikali cha Nation Front nchini Ufaransa amepigwa marufuku kushiriki kwenye kinyang'anyiro cha uchaguzi wa mabaraza ya miji, uliopangwa kufanyika mwezi Machi mwaka 2014, baada ya kumvunjia heshima Waziri wa Sheria wa nchi hiyo kwa kumfananisha na nyani.
Anne Sophie Leclere mgombea wa nafasi ya udiwani katika eneo la Rethel kwa tiketi ya chama cha Nation Front amezuiwa kushiriki kwenye kinyang'anyiro hicho baada ya kutoa taswira ya mtoto wa nyani kwenye ukurasa wake wa Facebook, akiwa na lengo la kumfananisha na Bi. Christiane Taubira Waziri wa Sheria wa Ufaransa mwenye asili ya Guinea. Chama cha National Front cha Ufaransa kinachoongozwa na Marine Le Pen hivi karibuni kimepata umashuhuri na uungaji mkono mkubwa wa wananchi wa Ufaransa kutokana na sera zake za kuwa dhidi ya wahajiri na kupinga siasa za Umoja wa Ulaya.
Inafaa kukumbusha kuwa, Cecile Kyenge Waziri wa Mshikamano wa Italia ambaye ni waziri wa kwanza mweusi, miezi michache iliyopita pia alikumbana na vitendo vya kibaguzi, baada ya Roberto Calderoli Naibu Spika wa Baraza la Seneti la Italia kumfananisha na nyani mwanamama huyo mwenye asili ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.