Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Saturday, October 19, 2013

Saudi Arabia kumkata kichwa hujaji wa Iraq


Saudi Arabia kumkata kichwa hujaji wa IraqHatua ya Saudi Arabia ya kutoa hukumu ya kukatwa kichwa hujaji wa Iraq, baada ya kukamatwa na askari wa Saudia kwenye makaburi ya Baqii, imekabiliwa na radiamali kali ya bunge la Iraq. Kamisheni ya Uhusiano wa Kigeni ya Bunge la Iraq imeeleza kuwa, hukumu hiyo iliyotolewa dhidi ya hujaji huyo wa Iraq inaonyesha jinsi utawala wa Saudia ulivyokuwa na chuki dhidi ya Waislamu wa Madhehebu ya Shia. Sami al Askari mjumbe wa kamisheni hiyo amesema kuwa, utawala wa Saudi Arabia hauna haki ya kutoa hukumu kama hiyo ya kukatwa kichwa hujaji huyo wa Iraq. Al Askari ameongeza kuwa, watawala wa Saudia wana chuki na uadui dhidi ya Mashia kutoka Lebanon, Iran, Iraq na hata wale walioko ndani ya nchi hiyo.
Ameongeza kuwa, nchi za Magharibi ambazo zimekuwa zikijinadi kutetea haki za binadamu zimekuwa zikifumbia macho  jinai na ukiukwaji wa haki za binadamu nchini humo, kwa vile watawala wa nchi hiyo ni vibaraka wa Magharibi.
Inafaa kuashiria hapa kuwa, Salam Kadhim hujaji kutoka Iraq alikamatwa na askari wa Saudi Arabia akiwa analia kwenye makaburi ya Baqii, ambapo mahala hapo wamezikwa watu wa Nyumba Tukufu ya Mtume Mtukufu SAW. Hukumu hiyo ya kukatwa kichwa, ilipangwa kutekelezwa mara tu baada ya kumalizika ibada ya hija.