skip to main |
skip to sidebar
41 wauliwa katika mashambulizi Sudan Kusini
Watu wasiopungua 41 wameuawa na wengine 63 kujeruhiwa katika
mashambulizi ya silaha yaliyotekelezwa katika jimbo la Jonglei mashariki
mwa Sudan Kusini. Ripoti za awali zinaeleza kuwa watu 41 wameuawa na
wengine 63 kujeruhiwa, huku hali ya baadhi ya majeruhi zikiwa mbaya
sana. Hussein Maar Kaimu gavana wa jimbo la Jonglei amesema kuwa kuna
uwezekano wa baadhi ya majeruhi ambao hali zao ni mbaya sana wakaaga
dunia wakati wowote. Maar ameongeza kuwa wavamizi walikuwa na silaha za
otomatiki na kwamba waliiba maelfu ya ng'ombe kwenye shambulizi hilo.
Kaimu gavana wa jimbo la Jonglei ambalo ni jimbo kubwa zaidi huko Sudan
Kusini amesema kuwa wanamgambo wanaoongozwa na David Yau Yau wanashukiwa
kuhusika na shambulio hilo.