skip to main |
skip to sidebar
Wazayuni waendelea na maneva ya kijeshi Palestina
Utawala wa Kizayuni wa Israel umeendelea kwa siku ya pili
mfululizo kufanya maneva ya kijeshi katika eneo la kaskazini mwa ardhi
za Palestina zinazokaliwa kwa mabavu. Taarifa zinasema kuwa, kikosi cha
ardhini cha jeshi la Israel ambacho tokea jana kilianza kufanya maneva
na luteka hiyo ya kijeshi katika eneo linalopakana na nchi tatu za
Syria, Lebanon na Palestina inayokaliwa kwa mabavu, yameendelea tena leo
kwa kutumia silaha mbalimbali, zikiwemo silaha nzitonzito. Taarifa
zinasema kuwa, milio ya milipuko ilisikika pia karibu na maeneo
yanayopakana na mashamba ya Shaba'a nchini Lebanon. Taarifa hizo
zimeelza kuwa, ndege ya kijasusi ya utawala wa Israel pia imekiuka
sheria za kimataifa kwa kuingia kwenye anga ya maeneo ya kusini mwa
Lebanon.