Jeshi la Sudan limepeleka askari zaidi huko Mashariki
mwa eneo la Darfur kwa lengo la kuimarisha usalama zaidi wa raia wakati
huu wa sikukuu ya Idil Adha.
Bilal Saed Daqis ambaye ni miongoni mwa maafisa wa Darfur
amesema kuwa, wanajeshi zaidi wamepelekwa mashariki mwa eneo hilo ili
kuzuia machafuko kati ya makabila ya al Manaliya na ar Razqat na
kuimarisha usalama zaidi.
Wakati hayo yanaripotiwa askari watatu wa kikosi cha
kulinda amani wa Umoja wa Mataifa UNAMID wanaotoka Senegal wameuawa
katika shambulio lililofanywa dhidi ya msafara wa umoja huko kwenye eneo
la Darfur. Mwakilishi maalumu wa kikosi cha UNAMID Mohamed Ibn Chambas
amesema kwamba, shambulizi hilo ni jinai na kwamba serikali ya Sudan
inapaswa kuchukua hatua muhimu ili kuzuia mashambulizi kama hayo.