Social Icons

rss feed facebook twitter google plus linkedin youtube email

Tuesday, October 1, 2013

WAFUNGWA WA KIISLAMU WAIFUNGULIA MASHTAKA SERIKALI YA UINGEREZA KWA KUWALISHA NYAMA YA NGURUWE



Kundi la wafungwa wa kiislamu takribani 200 limeishitaki serikali ya Uingereza kwa madai kwamba walikuwa wakilishwa Mikate, Keki na vyakula vingine
ambavyo ndani yake kulikuwa na nyama ya nguruwe.

Uchunguzi umefanyika katika vyakula vile vilivyokuwa na lebo ya 'halal' vikiwemo sausage, Mikate ya nyama na Keki, umebaini kwamba kuna asilimia 100 ya nyama ya nguruwe ndani ya vyakula hivyo. Bidhaa hizo zilibainika mapema mwaka huu jela ya HMP Sheppey Clusster huko Kent kusini mashariki mwa Uingereza.

Wizara ya Uingereza ya Haki ilithibitisha kuwa wafungwa 186 wameamua kuchukua hatua za kisheria dhidi ya serikali
kufuatia ugunduzi huo.

Wizara ya sheria imepokea idadi ya madai ya kiraia kufuatia ugunduzi wa chakula vilivyokuwa na lebo ya 'Halal' ndani yake kuwemo na nyama ya nguruwe. "Madai yote yatazingatiwa juu ya uhalali wake", alisema Jeremy Wright waziri wa Sheria.
Kwa mujibu wa takwimu rasmi, zaidi ya asilimia 13.1 ya idadi ya wafungwa nchini Uingereza ni Waislamu.

Waislamu ni haramu kula vyakula ambavyo ndani yake kuna nyama ya nguruwe, kwa maagizo ya Mwenyezi Mungu aliposema katika suratil Maidah aya ya tatu kwamba, "mmeharamishiwa mzoga na damu na nyama ya nguruwe....." 


No comments:

Post a Comment