skip to main |
skip to sidebar
Amnesty yakosoa ukiukaji haki za binadamu Saudia
Shirika la Msamaha Duniani (Amnesty International) limeikosoa
Saudi Arabia kwa kutokomesha hali ya kutisha ya haki za binadamu nchini
humo. Amnesty International imetoa ripoti iliyoiwasilisha kwa Umoja wa
Mataifa ikibainisha ukandamizaji na uvunjaji wa haki za binadamu dhidi
ya raia wa Saudi Arabia kama vile kutiwa mbaroni na kushikiliwa
kiholela, kukatiwa hukumu zisizo za kiadilifu na mateso mengine katika
kipindi cha miaka iliyopita. Amnesty International imewasilisha ripoti
yake hiyo kwa Umoja wa Mataifa kuhusu uvunjaji wa haki za binadamu
nchini Saudia Arabia kabla ya kuanza mkutano wa umoja huo uliopangwa
kufanyika hii leo Jumatatu huko Geneva Uswisi, kuchunguza hali ya haki
za binadamu huko Saudia. Ukandamizaji mwingine uliotajwa kwenye ripoti
hiyo ni kuhusu wimbi jipya la ukandamizaji dhidi ya wananchi huko Saudi
Arabia katika kipindi cha miaka miwili ya hivi karibuni.